[wanabidii] WATOTO WADOGO NA SHULE ZA BOARDING

Sunday, February 24, 2013
Shalom

Siku hizi imekuwa ni kama fasheni kwa wazazi kuwapeleka watoto wadogo
shule za kulala. Watoto wengine wanapelekwa huko wakiwa wadogo sana,
miaka minne au mitano. Huwa najiuliza sana, ni nini hasa
kinachopelekea wazazi kufanya uamuzi kama huo? Ni ubize au kwenda na
wakati? Wengine wanajitetea kuwa wanafanya kazi mchana kutwa na
wanarudi nyumbani usiku hivyo mtoto hashindi nao hivyo ni sawa tu
kumpeleka boarding, mimi sikubaliani na hili. Hata kama unarudi
nyumbani usiku angalau unaweza kupata muda wa kuongea na mtoto wako
na kuangalia afya yake na kujua anaendeleaje na sio kumpeleka shule ya
kulala na mnaonana mara moja kwa wiki au mwezi kabisa.

Mtoto anatakiwa ajifunze maadili ya familia yake na za kiMungu akiwa
na wazazi wake na afahamu jinsi ya kuishi na wazazi, ndugu, jamaa na
marafiki kwanza kabla ya kumpeleka kufundishwa na watu wengine? Je,
unadhani unamjengea nini mtoto wako kwa kumuacha kuishi na kulelewa na
watu tofauti wa wazazi wake katika umri mdogo kiasi hicho? Je,
unajuaje kama watoto wenzie hawamfundishi mambo yasiyofaa maana
haonani nawewe kila siku? Ni rahisi kugundua kama mtoto ana tatizo au
hofu fulani kama unakaa naye nyumbani kuliko kumuona mara moja kwa
mwezi.

Unafanya kazi kwa bidii kwa sababu ya maisha bora ya mtoto wako, sasa
kwa nini umjengee msingi mbovu kwa sasa kwa kisingizio cha kujenga
maisha bora ya baadaye? Mtoto umleaavyo ndivyo akuavyo, hata kama
umeenda kusoma mbali, ni vyema akikaa na mzazi mmoja kuliko kukaa
kwenye jumuia ya watu tofauti wenye maadili tofauti. Ni wakati sasa
wazazi tukabili na kutekeleza majukumu yetu hata kama ni magumu kiasi
gani na sio kuwasukumia watu wengine.

Kumbuka mtoto ana haki ya kudeka kwa mzazi wake japo isizidi sana,
sasa huko boarding atamdekea nani jamani???

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments