[wanabidii] TAARIFA JUU YA KIFO CHA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU EUSTACE NYARUGENDA NA KIUSALAMA INAYOMKABILI COSMAS MAKONGO

Sunday, February 24, 2013

MHUTASARI WA TAARIFA JUU YA KIFO CHENYE UTATA CHA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU MAREHEMU EUSTACE NYARUGENDA NA HALI TETE YA KIUSALAMA INAYOMKABILI MWANDISHI NA MTETEZI WA HAKI ZA BINADAMU COSMAS MAKONGO

 

Ndugu wanahabari, Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu umewaita baada ya kuona kwamba kuna umuhimu wa kufuatilia kwa karibu masuala yafuatayo: kwanza ni hali ya kiusalama na afya ya ripota wa kituo cha televisheni cha ITV, Cosmas Makongo. Pili ni kifo chenye utata cha mtetezi wa wa haki za wanawake Mkoani Mara Eustace Nyarugenda na mwisho ni kifo chenye utata pia cha mwakilisji wa redio ya kijamii, Redio Kwizera marehemu Issa Ngumba.

 

Mnamo tarehe 6 Disemba mwaka jana mtandao wetu uliwaiteni na kutoa taarifa jinsi ambavyo mwandishi Makongo alikuwa anapewa vitisho. Uchunguzi wetu wa awali ulioshirikisha asasi mwanachama wetu iliyopo mkoani Mwanza ya Wotesawa. Taarifa iliyoletwa na mkurugenzi wa asasi hiyo Bi Angela Benedicto ilionyesha kwamba kulikuwapo na umuhimu wa kufanya uchunguzi ili kufahamu nini kilichomsibu mtetezi huyo.

 

Hivyo basi Mtandao uliunda timu ya uchunguzi ambayo ilianza kazi yake Januari 03, 2013, ikiongozwa na Mratibu wa mtandao Onesmo Olengurumwa, na afisa usalama Benedict Ishabakaki, wawili hawa walitokea Dar es Salaam na wakashirikiana na mashirika wanachama Mkoani Mwanza.

 

Lengo kuu la uchunguzi huo ililikuwa ni kuchunguza aina ya vitisho alivyokwa anavipata Makongo na kisha kutafuta njia ya kumhakikishia usalama wake. Zaidi ya hapo ripoti hii ilidhamiria kutafuta namna ya kumjengea uwezo ili kufanikisha majukumu yake ya kila siku. Mtandao wa watetezi ulitaka kufuatilia na kujua aina ya vitisho alivyokuwa anavipata kutokana na kazi yake kama mwandishi. Vile vile Mtandao ulilenga kufahamu mazingira yake kwa sasa kutokana na vitisho, hatima yake kikazi, afya yake na vile vile kutafuta njia za kumsaidia kwa matibabu.

 

Tulichokishuhudia

 

(i)  Hali yake kiafya

 

Tulipomhoji alisema kwamba ilikuwa mnamo tarehe 28 Oktoba mwaka jana alipoanza kujisikia vibaya, mwili wake ulikuwa ni mchovu baada tu ya kuwa ametangaza tukio la mauaji ya watu na mifugo yaliyotokea huko Biharamulo, Ngara na Muleba. Moyo wake ulianza kwenda mbio akawa anapumua kwa shida na kusikia maumivu makali ya kichwa. Wakati uchunguzi huo ukiendelea alikuwa bado anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, mpaka sasa vipimo vimeshindwa kuonyesha hasa ugonjwa unaomsumbua.

 

(ii) Vitisho kwa maisha yake

 

 

1


Kwa sababu baadhi ya waathirika wa habari anazozitoa Makongo ni viongozi wa serikali na hata baadhi ya watu binafsi wenye nafasi nzuri kiuchumi, kwa hiyo maisha yake yamo hatarini. 2 Anasema ameshuhudia kwamba kila atoapo taarifa za kiuchunguzi amekuwa akipata vitisho mara kwa mara na vimekuwa vikija katika staili tofauti tofauti. Kwa mfano manmo Disemba 2012 alipata vitisho kupitia kwenye simu yake ya mkononi, vitisho hivyo vimekuwa vikitoka katika simu zisizosajailiwa na baadhi ya vitisho vilifika kama ifuatavyo;

“umetufuatilia kwa muda mrefu na sasa unafikia mwisho wako…Ujumbe mwingine ulisomeka hivi “Makongo wewe ni kikwazo kwa watu wengi, tutahakikisha tunakushughulikia…”

Makongo anasema mara baada ya kuripoti mauaji ya mifugo na na watu huko Muleba, Kagera mwezi Juni 2012 alianza kupata vitisho kutoka kwa baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi hali iliyomlazimisha kuhama eneo hilo kwa muda. Kwa hali yoyote ni vigumu kusema mtetezi huyu yupo katika hali ya usalama kwa sababu ni vigumu kutabiri ni lini maadui zake wanaweza kumdhuru.

 

Anasema bado anapokea vitisho na mfano mzuri wa kuthibitisha hilo ni mnamo tarehe 16, 2012 pale alipofikishwa katika Hospitali ya Bugando ambao baadhi ya madaktari hawakuamini kwamba kweli anaumwa na badala yake walikisia kwamba labda yupo katika kazi zake za uchunguzi. Kwa sasa amekuwa mwoga kutokana na mazingira hayo hali yake kiafya siyo nzuri anahitaji matibabu, usafiri, na ada kwa ajili ya watoto wake kwa sababu kwa sasa hana kipato kutokana na maradhi yanayomkabili.

 

Mapendekezo yetu.

 

       Waandishi wote wanahitaji wapatiwe mafunzo ya usalama

       Wamiliki wa vyombo vya habari wanatakiwa kuwa na mafungu ya pesa ya dharula kwa ajili ya kuwasaidia waandishi pale wanapopata matatizo.

 

       Taasisi za vyombo vya habari kama vile Taasisi ya Uhuru wa Vyombo vya habari Kusini mwa

Afrika (MISA-Tan) Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), kushirikiana na Mtandao wa Watetezi popote walipo katika majukumu yao.

 

       Mtandao unawashauri wamiliki wa vyombo vya habari kuwathamini waandishi wawapo katika hali zote katika afya na katika matatizo yao pia.

 

       Kwa vile mpaka sasa imekuwa vigumu kuufahamu ugonjwa unaomkabili Makongo ni vyema apelekwe katika hospitali zenye uwezo zaidi wa kutambua magonjwa ya kipekee.

 

       Pia tunawaomba watu wote wenye mapenzi mema na watetezi kutoa msaada kwa familia ya Bw. Makongo katika kipindi hiki cha ugonjwa wake.

Habari njema kiasi

Hata hivyo wakati tulipokuwa katika maandalizi a mwisho ya taarifa hii Makongo alitufahamisha kwamba ameanza japo kwa kujikongoja kujaribu kufanya kazi na jana alirusha taarifa katika kituo chake cha kazi (ITV).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

2


3

 

 

KIFO CHA EUSTACE NYARUGENDA

 

Mtandao wetu pia ulifanya uchunguzi wa kifo cha mtetezi wa haki za binadamu na mkurugenzi mtendaji wa shirika la Action Based Foundation (ABC), lilipo Musoma Eustace Nyarugenda ambaye alikuwa akiongoza mapambano dhidi ya ukatili wa wanawake Mkoani Mara. Mtetezi huyo alifariki tarehe 5 Disemba mwaka jana baada ya kuwa imetangazwa kwamba amepotea kwa siku tatu.

 

Mtandao ulituma timu ya watu wanane chini ya mwamvuli wa Mtandao wa Watetezi na wawakilishi wetu waliopo katika Kanda ya Ziwa. Uchunguzi wetu umebaini kwamba Nyarugenda alijitengenezea maadui kutokana na kazi zake ambazo kwa kiwango fulani zilihusu kuingilia maisha ya familia za watu wengine wakati akitetea haki za wanawake.

 

Shughuli zake za kupinga ukatili majumbani na unyanyasaji wa wanawake zinatajwa kuwa chimbuko la la uadui na watu wengine. Mkewe na ndugu wa karibu walipata kumshauri kwamba shughuli zake siyo tu kwamba zilikuwa zinahatarisha uhai wake bila pia hata wa ndugu zake na hata wafanyakazi wenzake. Kuna wakati marehemu alipata ujumbe kutoka kwa mtu aliyejifanya kwamba ni mwanamke. Hiyo ilkuwa ni muda mfupi mara baada ya kuwa ameshughulikia mgogoro wa kifamilia wa mtu fulani. Ujumbe huo wa Kiswahili ulisomeka hivi

 

Halo tukutane Jumba la Dhahabu mimi Asha”.Jumba la dhahabu ni maneo ya Musoma yanatumika mara nyingi kufanya uhalifu.

 

Siku tatu kabala ya kupotea kwake Nyarugenda ni kama alitabiri kifo chake pale alipomwambia ofisa wake aitwaye Marwa “tuna vita vikubwa mbele yetu tunatakiwa kujipanga” Kwa ujumbe huu, anasema Bw. Marwa ni kama vile marehemu alitabiri kifo chake lakini aliogopa kuwavunja moyo wenzake.

 

Kupotea kwa mara ya kwanza 2011

Ripoti ya timu ya uchunguzi inaonesha kwamba mnamo mwaka 2011 Nyarugenda alipotea na kuonekana baada ya siku nne katika kijiji cha Gangabalili Bariadi mnamo Agosti 4, 2011. Mtoa habari wa tukio hilo alimuona Nyarugenda akishushwa kutoka kwenye gari aina ya Escudo, akiwa hajitambui na mikwaruzo na uvimbe katika ulimi.

 

Kupotea kwa mara ya pili Disemba 2012

Tuligundua kwamba Nyarugenda alipotea tarehe mbili Disemba baada ya kuwataarifu wenzake kwamba anakwenda Tarime. Na baada ya siku mbili ndipo alipatikana katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Savannah mjini Bunda. Mara baada ya tukio hilo tulimtuma mwakilishi wetu mkoani Mara afuatilie jambo hilo. Taarifa hizo zinasema kwamba Nyarugenda alikutwa akiwa hajitambui na kwamba mezani katika chumba alicholala kulikuwapo na bia aina ya Castle Milk Stout na sumu ya kuulia wadudu aina ya DDT. Alifariki akiwa njiani akiwa anapelekwa katika Hospitali ya Wilaya Bunda.

 

Hitimisho na ushauri wetu.

 

Tumejiridhisha kwamba Nyarugenda alipoteza maisha kutokana na kazi zake za utetezi wa haki za binadamu. Hata kama ni kifo kilichopangwa au ni kwa kudhamiria kujiua, yote yatakuwa ni kwa sababu alikutana na mazingira magumu yaliyokuwa yanamkabili.

 

Kwa  upande  mwingine  mtandao  haujaridhishwa  na  utendaji wa  kazi wa  Jeshi la  Polisi kulingana  na

 

 

3


sauala hili. Mtakumbuka kuwa mwaka jana mara baada ya kifo chake tulitoa tamko la pamoja na wenzetu wa Kanda ya Mashariki na Pembe ya Africa na kulitaka Jeshi la Polisi kuchunguza kifo hiki4 kwa haraka. Ila uchunguzi huu umebaini kuwa kumekuwapo na ucheleweshaji na ugumu katika utoaji taarifa za kifo hiki. Miezi miwili tokea kifo hicho bado hawajatoa taarifa za uchunguzi wa kifo hicho. Na wanajenga hoja kwamba sampuli bado zipo ofisini kwa Mkemia Mkuu wa Serikali katika kituo cha Mwanza kwa ajili ya uchunguzi. Mtandao wetu ulifika katika ofisi za Mkemia Mkuu kwa ajili ya kujiridhisha kama weli sampuli hizo zipo na baada ya kufika hapo tulifahamishwa kwamba hakuna sampuli zozote zilizokwishafikishwa hapo hapo kwa ajili ya uchunguzi.

Hali hii inatufanya pia tuhoji utendaji wa kazi wa jeshi hilo hasa katika upelelezi wa matukio yanawahusu wanaharakati kama vile Dkt Stephen Ulimboka. Wakati huo huo tunawafahamisha kwamba Taasisi ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-Tawi la Tanzania (MISA-Tan) lilihusika na uchunguzi wa kifo cha mwakilishi wa Redio Kwizera, Issa Ngumba ambaye mwili wake uliotelekezwa porini uliokotwa tarehe 8 Januari, kwa vile Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi wake tunaomba tusiliongelee suala hilo na tutafanya muda muafaka ukifika.Pamoja na hayo uchunguzi wa MISA-Tan umebaini kuwa kwa sasa waandhishi wa habari hapa nchini wapo katika mazingira hatarishi muda wote.

 

Mapendekezo yetu

 

Kutokana na uzoefu wetu wa masuala haya mawili yaani kifo cha Nyarugenda na vitisho kwa Makongo, tunashauri kwamba serikali iandae mazingira bora ya kazi kwa watetezi ili waweze kufanya kazi bila vitisho vya aina yoyote kutoka kwa watu wanaojihusisha na uvunjifu wa haki za binadamu.

 

Jeshi la Polisi liache kufanya ubaguzi katika kufuatilia matukio ya kupigwa, kutishiwa ama kuuwa kwa watetezi wa haki binadamu. Watambue kuwa wao ndio wenye jukumu la msingi la kuwalinda watetezi wa haki za binadamu hapa nchini.Hivyo basi baada ya tamko hili tunalitaka jeshi la polisi mkoani Mara wafuatilie kwa undani kifo cha Nyarugenda.

 

Tunashauri kwamba watetezi wote wa haki za binadamu wapate mafunzo katika usalama wao na pia kisa cha Makongo kinatufanya tuwaombe wamiliki wa vyombo vya habari watoe kila aina ya msada kwa watumishi wao mara wanapopata matatizo.

 

Tunawatakieni kazi njema

 

 

 

 

Onesmo Olengurumwa

 

Mratibu wa Kitaifa –Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania

 


--
www.wejobs.blogspot.com Jobs in Africa
www.jobsunited.blogspot.com International Job Opportunities

--
Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments