KABILA lina DINI,ina SALA,MATAMBIKO ambayo kwa kupita LUGHA hii ya Dini wanawasiliana na Mungu wao ambaye wanaamini kwa kuongea Lugha hiyo,kwa kufanya mambo hayo kwa Lugha hiyo basi wanasikilizwa.Mie naongelea kabila(Kanisa) ambalo nalifahamu zaidi.Kanisa Katoliki ni kama KABILA FULANI...wana lugha yao,wana alama zao,wana rangi za ibada, wana ishara zao na hizi ni tamaduni za UNIQUELY kwa KATOLIKI...mfano wa utamaduni wa Wachaga,wahehe,n.k!Sasa kama haujui tamaduni hizi,hauwezi kuzichallenge eti ni mbaya..Kwanini ni mbaya kwako?Ni kwa sababu si mmojawapo wa Ukoo huu au lugha na jamii hiyo.Ukitaka kufahamu,ingia,jifunze lugha yao na hatimaye uelewe.Si mtu anaenda China anakuwa maandishi fulani,anaanza oh..mbona hakuna A,B na C!!!Hili si swala lao,ni lako kwa kushindwa kujifunza na kuelewa lugha hiyo.Ndiyo maana ndugu zangu,vita ya DINI haiwezi kuisha kama hatutafahamu tofauti hizi.Kanisa Katoliki linafundisha kuhusu ECUMENISM-Yaani mahusiano mema na madhehubu ya Kikristo kuwa Kama haujui maana ya EKARISTI TAKATIFU,usijisumbue kunichallenge maana imo kwenye CULTURE YANGU na si yako.Kama mie sijui UPAKO kwa nini nikusumbue?Pia kuna kitu kinaitwa.INTER-RELIGIOUS DIALOGUE... Hii ni kwa mahusiano na DINI tofauti na Kikristo,hapa ni kwa doctrine zaidi...Mfano kama hauamini kuwa KRISTO ni Mungu ila mie naamini shida yako nini?Maana ni utamaduni wangu.
SASA Hapa wale wanaoliona Kanisa Katoliki kama adui,wanaona kama vile wanatumia elimu yao kuzima UENJILISHAJI WAO WA MIPASHO against RC.Si hivyo ndugu tuelewe lugha.
Mfano;Humu ndani kuna watu huko kwao majina yao ni MATUSI kwa makabila mengine...je,nisiite jina hilo kwa sababu tu ni tusi kwa kabila jingine?Na je,jina la tusi kwa kisukuma mbona ni jina la Mungu kwa Wahaya?Mbona jina la mtu na lenye maana njema kwa wasukuma mbona ni Jina la mnyama kwa WAHA?Jamani tukubaliane kuwa DINI NI LUGHA,na hauwezi kuchallenge lugha ya mtu kuwa ni mbaya maana hauijui.Jifunze kwanza::::UKITAKA KUJUA UTAMU WA NGOMA,INGIA UCHEZE.
-- Jobs in Africa - www.wejobs.blogspot.com
International Jobs - www.jobsunited.blogspot.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments