Kila siku nchini petu hukosi kukutana na mambo ambayo yatakushangaza
pakubwa ukiwa wewe ni Muislam unaejitambua. Gazeti la leo la Mwananchi
(Jumatatu, Februari 17 2014) uk. wa 3 kuna makala, ''Wasomi waianzia
Rasimu ya Katiba Dar.''
Makali hii inaeleza kuwa wasomi na wanazuoni wapatao 300 wanakutana
Dar es Salaam kujadili Rasimu ya Katiba.
Wasomi hawa katika yote hofu yao iko katika Uislam.
Wanauliza vipi Zanzibar ambayo ni nchi ya Waislam wengi kupita kiasi
itajiepusha na udini?
Hapa ndipo palipo cha kushangaza.
Hivi huu udini ulifurtu ada Tanzania Bara hawa wasomi na wanazuoni hawauoni?
Wao wenyewe katika hicho kikao chao hawajioni kuwa wako Wakristo watupu?
Imekuwaje ikawa hivyo?
Mbona hawajajiuliza vipi wao watajiepusha na udini?
Lakini Waislam tujiulize kweli hii ni agenda ya kutia hofu udini wa Zanzibar katika
serikali tatu ni agenda yao hawa wasomi au kuna mtu anaikoleza kwa kuilipia?
Tujiulize swali lingine. Kwani Uislam kuwa na nguvu Zanzibar hairuhusiwi?
Haiyumkiniki ikawa leo Wazanzibari watatishwa na Uislam unaoshamiri katika
jamii.
Huyu anaetishwa na Uislam Zanzibar kiasi cha kukosa usingizi ni nani?
Waarabu wana msemo, ''Ukiijua sababu ile ajabu inaondoka.''
Kumbe siku zote hizi vurugu zote na mauaji Zanzibar wizi wa kura nk. nk.
kinachowatisha ni kuwa utaingia uongozi ambao utaharibu na kuvuruga maslahi
ya Kanisa....
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments