Mvua kubwa inaendelea kupiga/kunyesha maeneo yote hapa jijini, changamoto kubwa iliopo nadhani wengi tuishioa hapa twaijua, tuna miundombinu mibovu sana ya maji na bara bara kati kati ya jiji, kwa leo mjini kwenda ni tatizo kwani magari hayatembei na wale watembea kwa miguuu wawe na pesa za nauli ya ziada za kubebwa kuvushwa ktk madimbwi makuubwa.
hatar sana dar mvua ikinyesha, sjui maeneo ya mabondeni leo hali yao ikoje? sjui wale wafanyabiashara ndogo ndogo wanaopanga bidhaa zao chini, ni vurugu tupu mvua ikinyesha dar
nini kifanyike kuondoka kero hizi? serikali, wakaazi na wafanyabishara, nini kifanyikie, au tupeleke ktk bunge la katiba nalo hili maana sku hizi mtu akiibuka tu, oooh peleka Dodoma
0 Comments