Wakati polisi wa Tanzania wakifanya mazoezi ya kupambana na kuzuia uhalifu (ugaidi?) hotelini "jijini Mwanza", polisi wa Japan wafanya mazoezi kama hayo kwenye viwanja vya ndege, na bandarini.
Kwakweli mazoezi ya waJapan nadhani yamefanywa kwenye sehemu "nyeti" ukilinganisha na hoteli iliyopo "uswahilini".
Polisi wa Japan walikuwa na vifaa rasmi (nguo za kujilinda na vitendea kazi) na usafiri wa magari na helikopta; wakati hapa kwetu "walitumia" magari yao ya kawaida "defender" ambazo nyuma zipo wazi!!
Fikiria hapa Tanzania, watokee wahalifu wa ukweli wenye silaha hatarishi, "hawa askari wa polisi tunaowaona kwenye defender ambao hata hawavai bullet proof vest kweli watathubutu kuwasogelea? Tatizo jingine "foleni". Hata kama kuna uhalifu sehemu, wahalifu wanaweza kutokomea au kufanya uhalifu wao kabla ya kufikiwa na polisi.
Huko, Japan; kwenye bandari walitumia boti na helkopta kukabiliana na "askari wenzao waliokuwa wanaigiza kama wahalifu".
Kwenye kiwanja cha ndege; afisa uhamiaji walipewa purukushani ya kupambana na "mhalifu" aliyekuwa na kisu "hand-to-hand combat" (siyo kutumia bunduki (^_^)).
Pia walifanya mazoezi ya njia salama ya kuhifadhi "mzigo" unaosadikiwa kuwa na bomu kuuweka kwenye mtungi maalumu ili usijekuleta madhara. Walikuwa na vifaa vya kujilinda na milipuko!
Mungu ibariki Tanzania tuendelee kujifunza zaidi, na tuelimike kuhusu elimu ya usalama. Hii itasaidia kuifanya sekta hii kuwa ya kipaumbele siku za usoni.
Chanzo: NHK World (kipindi kwenye TV)
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
KARIBU MABADILIKO MPYA: Jukwaa hii sasa linapatikana katika mwuonekano wa Kisasa: www.mabadiliko.com tafadhari tembelea na jisajili huko
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments