[wanabidii] Taarifa sahihi kuhusu kusimamishwa uongozi kwa m/kiti na katibu chadema wlaya ya magu

Monday, February 17, 2014
Kutokana na kile kilichoandikwa katika mitandao ya kijamii kuhusu kufukuzwa uongozi kwa mwenyekiti na katibu wa chadema wilaya ya Magu, tunahitaji kuweka kumbukumbu sawa kuwa hakuna hata kiongozi mmoja kati yao aliyefukuzwa Uanachama kwa tuhuma ya kuwa katika mtandao wa zitto, au kwa shinikizo na agizo toka kwa Katibu Mkuu.

Uongozi wa kanda ya Ziwa Magharibi unapenda kuutaarifu umma kuwa viongozi hawa wamesimamishwa nyadhifa zao na kikao halali cha chama ngazi ya wilaya kilichoketi tarehe 15/2/2014 hapo wilayani Magu. Hata hivyo upotoshaji huo ulikuwa na lengo la kupaka matope maamuzi halali ya chama. Hatua hii imechukuliwa na kikao halali cha kikatiba mara baada ya viongozi hawa kushindwa kabisa kutimiza majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kushindwa kutekeleza programu mahususi ya Chadema ni msingi kama yalivyo maelekezo ya chama nchi nzima. Hata hivyo wakati wa ziara ya Katibu Mkuu katika kanda ya ziwa magharibi iliyofanyika tarehe 1/2/2014 viongozi hawa walipoombwa kuwasilisha ripoti ya CDM ni msingi, wakiri wazi kuwa hawajatekeleza zoezi hilo tangu kuanzishwa kwakwe kwa takribani ya miezi 6 sasa, pamoja na kuendelea kupokea ruzuku ya chama kwa ajili ya kazi hii, hakuna kilichokuwa kikifanyika, kitendo hiki kilitafsiriwa na wanachama na Wadau wa chama Magu kuwa ni uzoroteshaji wa maendeleo ya chama.

TUNATAKA IELEWEKE WAZI KUWA HAWA VIONGOZI WAMESIMAMISHWA NYADHIFA ZAO NA HAWAJAFUKUZWA UANACHAMA KAMA ILIVYO RIPOTIWA.

IMETOLEWA NA OFISI YA CHADEMA KANDA YA ZIWA MAGHARIBI.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Related Posts

0 Comments