[wanabidii] KWA WANAMAPINDUZI NA UKAWA (WOTE NI WANABADILIKO) BUNGE NI CHACHU KWA MAENDELEO:

Wednesday, November 18, 2015
KWA WANAMAPINDUZI NA UKAWA (WOTE NI WANABADILIKO) BUNGE NI CHACHU KWA MAENDELEO:
Nimekuwa nikiwa kimya kwa kipindi kuhusu mchakato wa Uspika wa Bunge la 11 la JMT. Kwasababu Spika amekwisha patikana, na Naibu Spika atapatikana ndani ya masaa 72. Ninadhani kuna haja ya kuzungumzia kidogo na kutoa maoni yangu.

Kwanza kabisa kazi ya bunge ni kutunga sheria, kusimamia utendaji wa serikali na kuishauri serikali. Katika kutimiza malengo haya pamoja na Serikali, na Mahakama, bunge huchukua sehemu muhimu kabisa katika kuhakikisha utendaji wa serikali unakuwa katika hali ya utendaji wa viwangu, na wenye tija.

Nimekuwa nikitazama, mihimili mitatu ya dola (Serikali, Bunge na Mahakama) kama mihimili ambayo inatakiwa kufanyakazi kwa pamoja ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo ya kijamii, uchumi, kisiasa na utoaji wa haki. Ili utendaji kazi wenye tija uweze kutokea kuna wanazuoni wanakubaliana kuwa mihimili hii mitatu inapaswa kuwa huru na isiyoingiliwa na mihimili mingine...lakini pia wanakubaliana kuwa vyombo hivi havina utendano na mipaka ya kuingilia mihimili mingine wa moja kwa moja (kwa tafsiri ya haraka haraka ya maneno There is no absolute separation of power.

Mwanasiasa  mashuhuri Zitto Zuberi Kabwe ametoa maoni yake hivi karibuni kwamba kitendo cha Serikali kuonekana kuingilia mchakato wa upatikanaji wa Spika siyo ukuaji wa demokrasia...na kusema ni kana kwamba serikali inapanga nani awe Spika, na nani awe Naibu wa Spika...

Kwa mtazamo wangu tofauti na wa Mh. Zitto Zuberi Kabwe ni kwamba Mihimili hii inahitaji kufanya kazi yake vizuri.. chukulia mfano wa gari.. gari ni muunganiko vya mifumo mbalimbali na mifumo hii isipofanya kazi kwa pamoja gari haiwezi kufanyakazi ipasavyo: Ninafananisha Mfumo wa Injini ya Gari na Serikali, Mfumo wa Gearbox na Bunge, Mfumo wa Break na Mahakama... Ikiwa injini itakuwa inafanya vizuri lakini gear haziingii, au zikiingia inaruka kutoka gear numba moja hadi tatu mara gear inachomoka na kuwa free...ninadhani gari hili litakuwa lina taabu kubwa sana kwa mwendeshaji...au ikiwa mifumo ya injini na gearbox ikafanya vizuri halafu Mfumo wa Break ukawa ni mbovu na hilo gari likawa limeanza kutembea vizuri kwa sababu mfumo wa injini na gearbox vinafanya vizuri inatarajia hata kama dereva wa gari hilo atakuwa ni mtaalamu kiasi gani wakati wowote anaweza kuliangusha gari hilo na kuleta madhara...

Kutokana na mfano huyo wa gari..ninarudi na kusema kwamba Serikali kikatiba inamipaka yake katika utendaji..lakini ikiwa serikali inatamani nani akisimama kwenye kiti cha Uspika au Unaibu wa Spika watatenda kazi zao vizuri basi ni njambo jema sana kwani ili dhana ya Hapa Kazi Tu iweze kufanyakazi vizuri pia ni vyema kwa mifumo yote kuweza kufanyakazi vyema pasipo mfumo mmoja kuwa kikwazo katika utendaji wa mfumo mwingine... ndiyo ninarudi kwenye yale maneno kwamba: In the state organs there is no absolute separation of power...and if there is no absolute separation of power therefore there should be relative separation of power.

Bunge kwa ujumla linaweza kwenda vizuri ikiwa wabunge wote watakuwa katika hali ya kutaka kuhakikisha kuwa serikali inafanyakazi zake vizuri...kuisimamia na kuishauri.. hakuna sehemu katika inasema, au desturi na kanuni za bunge zinasema kazi ya bunge ni KUKWAMISHA UTENDAJI WA SERIKALI.. japo kuwa bunge linaweza kufanya hivyo..lakini wakiweza kufanya lobbying vizuri ndani na nje ya serikali pamoja na ndani na nje ya kambi mbalimbali za mbungeni yaani Chama Tawala na Upinzania Bunge linaweza kufanikisha agenda zake vizuri..hii ndiyo siasa ya karne ya 21 katika nchi ya kiafrika...na Tanzania tumeonyesha ukomavu wa kisiasa kutokana na uchaguzi tuliofanya mwaka huu wa 2015.

Wabunge, Naibu wa Spika na Spika wa bunge la JTM wakitambua kuwa wanamapinduzi, au wanamabadiliko kwa rangi zao kote duniani wamefanikiwa kuleta mabadiliko wanayoyataka kwanza KWA KUJIFUNZA NA KUKUBALI KUWA NA UVUMILIVU WA KISIASA, pili KUTAMBUA KUWA SI WAKATI WOTE MAONI AU HOJA ZAO ZITAKUWA NI BORA KULIKO HOJA WA UPANDE WAPILI, tatu WAPINZANI PAMOJA NA CHAMA TAWALA WOTE TUNA-CUSTODY NA UZIMAMIZI WA RASILIMALI, UTAMADUNI, DESTURTI, NA USTAWI WA JAMII YA WATANZANIA KWA UJUMLA KATIKA NYANJA ZOTE ZA KIUCHUMI NA KIDEMOKRASIA.

JONATHAN N'HANDI MNYELA
MCHAMBUZI WA MAMBO YA KISIASA NA MAENDELEO YA JAMII

--
Jonathan N'handi Mnyela
P. O. Box 3385
Dar es Salaam
Tanzania
Alternative email: jmnyela@yahoo.com
Blog: www.mnyela4consultation.wordpress.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments