1. Gari yake haijaharibika kabisa na tunaaambiwa iliacha njia na kupinduka tunajua sababu kubwa ya magari kuacha njia ni kupasuka kwa matairi lakini hili gari la Mchungaji Mtikila hakuna tairi liliposuka. Sasa tuambiwe sababu ya kuacha njia na kupinduka ni nini?
2. Mchungaji mtikila hana alipoumia au kubleed damu.(Labda iwe kafa kwa mshtuko wa moyo au internal wounds. Kwenye picha anaoekana hajaumia hata kidogo hata nguo alivozavaa zikiwa hazijachanika hata kidogo.Sasa tuambiwe sababu gani nyingine iliyopelekea kifo chake?
3.Tunaambiwa ajali alipata SAA 11 alfajiri Chalinze kwaa asili ya eneo la Chalinze ni eneo bize sana kwanini picha iliyosambaa inaonesha ninasubuhi kabisa kumekucha ina maana ajali yake haikushtukiwa na watumiaji wengine wa Barabara mpaka asubuhi.
Angalizo sijamlaumu mtu yeyote kwenye hii ajali ila ni maswali ambayo nilikua najiulza binafsi sasa nawaomba msichafue hali ya hewa.
0 Comments