[wanabidii] Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa wangu...

Sunday, October 04, 2015
Mwanakijiji

    Hakuna mwanasiasa yeyote nchini tangu uhuru ambaye amepigania haki za kiraia na kushinda kama Christopher Mtikila. NInaamini historia itakuja kumkumbuka kama shujaa wa demokrasia kwani pamoja na yote ambayo amepitishwa ameendelea kusimama kudai haki za raia wa Tanzania kwa namna ambayo mahakama zimekuwa upande wake mara ZOTE!

    Leo hii napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mtetezi huyu wa haki za raia. Ni mwanasiasa pekee ambaye amefanikiwa kulazimisha serikali kufanya isiyotaka kufanya na hata ilipokataa kufanya ametuwezesha kuona kuwa serikali haitaki kwa sababu tu haipendi si kwamba hoja ziko upande wake. HE IS MY HERO!

    Ukweli ni kuwa amewapita kwa mbali sana wale wanasiasa wetu ambao labda majina yao ni maarufu sana na ambao wanaonekana ni maarufu; siyo tu Mtikila anazungumza anachozungumza bali anafanya pia anachozungumza.

Of course, haiondoi ukweli mwingine wa mapungufu yake au siasa zake lakini ukweli ni kuwa kila alipojaribiwa na watawala amewashinda. Rekodi yake ya ushindi kwa miaka ishirini na ushee sasa inasimama kama ushahidi wa ushujaa wake.
 
  Inasikitisha haijatokea wanasiasa wengine wa upinzani hata mara moja kuwa sehemu ya kesi zake au kuonekana wanajiingiza kama friends of the court (amicus curiae) kuonesha wanaunga mkono hoja zake.
 
    When it comes to the 'walking', Rev.Mtikila does the walk!

Share this :

Related Posts

0 Comments