THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT'S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametuma salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Chifu Abdu Adam Mkwawa, ambaye aliaga dunia jana, Jumamosi, Februari 14, 2015 hospitalini mjini Iringa.
Katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza leo, Jumapili, Februari 15, 2015, Rais Kikwete amesema kuwa amesikitishwa na kushtushwa na kifo cha Chifu Mkwawa ambaye amemwelezea kama "Chifu mnzuri, kiongozi na mtu wa watu, ambaye katika maisha yake yote alihangaika kuenzi na kudumisha kumbukumbu za utamaduni wa Mkoa wa Iringa, za machifu wa mkoa huo na utalii wa Iringa."
Rais Kikwete amemweleza Mheshimiwa Masenza: "Nawapeni pole sana na naungana nawe, familia ya marehemu na wananchi wote wa Mkoa wa Iringa katika kuomboleza maisha ya Chifu na kiongozi ambaye tutaendelea kumkumbuka kwa mchango wake katika kujenga na kuendeleza mahusiano mazuri ndani ya jamii. Aidha, naungana na familia katika kumwomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Abdu Adam Mkwawa. Amen."
Wakati huo huo, kesho, Jumatatu, Februari 16, 2015, Rais Kikwete ataungana na wananchi wa Mkoa wa Iringa katika mazishi ya Marehemu Mkwawa.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments