[wanabidii] MAJIBU YANGU JUU YA HOJA ZILIZO KATIKA TAMOKO LA UKAWA JUU YA "MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA YANAYOENDELEA BUNGE MAALUM LA KATIBA"

Friday, August 15, 2014
Kutokana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na UKAWA juu ya "Mchakato wa Katiba Mpya na Yanayoendelea Bunge Maalumu la Katiba". Taarifa hii imejaa upindishaji wa hali halisi ili kukidhi matakwa ya kundi la UKAWA kwa kujivika jukumu la kutoa hukumu (to be judgemental) juu ya kile kinachoendelea huku wakijiweka katika viatu vya watanzania ambao hata hivyo hawajawahi kuomba ridhaa ya Watanzania au kama wanawafamu vyema au kama wanachokipigania ni kwaajili ya maslahi ya Watanzania au yale ya kwao na vyama vyao.

Kabla sijaichambua na kujibu hoja zao za msingi kwanza ninahitaji kuweka bayana na kwa mapana kile nilichokisema katika aya iliyotangulia hapo juu kuhusu haya: (i) Kutoa hukumu (to be judgemental) na (ii) kujiweka katika viatu vya watanzania; kama ifuatavyo:

Kutoa Hukumu (to be Judgemental) juu ya Mchakato unavyoendelea: Tukumbuke kuwa kundi la UKAWA imeundwa na vyama vya siasa ambavyo kwa kimoja kimoja huwa na lengo la siku moja kuchukua dola na kutawala kwa kuzingatia taratibu za kidemokrasia. Hivyo tusitegemee hata siku moja maoni au tuhuma ambazo zitatolewa kutoka kwao dhidi ya chama tawala zitakuwa na ukweli usiokuwa na shaka wala mawaaa. Sasa, kwanini kundi la UKAWA halina uhalali wa kutoa hukumu hii juu ya Chama kingine cha Siasa, yaani CCM?.. Jibu ni rahisi sana hivi vyote ni vyama vya siasa, hivyo hakuna sehemu iliyo sawia (neutral ground) kwa upande wowote kuweza kusema kuwa kina mtazamo sahihi kuliko upande mwingine, hasa ukikumbuka vyama vya siasa lengo lao kuu ni siku moja kuja kutwaa dola na kuongoza serikali. Binafsi, nilitarajia kuona Taasisi za Kidini, na Kiraia zikitoa hukumu/ tuhuma hizi, ikiwa CCM wamekuwa wakinajisi mchakato wa Katiba Mpya kwa njia moja ama nyingine. Ninashawishika kuchagua Taasisi hizi kwa sababu moja  tu, ambayo ni kuwa Taasisi za Kidini na zile za Kiraia, hazina muegemeo wa moja kwa moja kuhusu siasa hii ya Katiba Mpya au kutetea matakwa na maslahi ya kisiasa ya Chama fulani au Vyama fulani vya Siasa kwa njia moja ama nyingine.

Kujiweka katika Viatu vya Watanzania: Ikumbukwe kuwa UKAWA imeanza wakati wa mkutano wa kwanza wa Bunge Maalum la Katiba. Hivyo hawana uhalali kutoka wa wananchi ambao wamekuwa wakijipiga vifua kuwa wanawawakilisha. Mfano. Wakati wa Mkutano wa Kwanza walikaa kwa takribani siku 30 wakitunga kanuni na siku za mwishoni kabisa ndipo walipotoka nje ya Bunge na kususia, kwanini wasingetoka mapema zaidi ya hapo? yaani baada ya kutumia pesa za Watanzania ndipo walipotoka. UKAWA imekuja kwaajili ya kuunganisha nguvu za baadhi ya vyama vya siasa, hasa hivi vyinavyojii kuwa ndiyo vyama vikuu vya upinzani, ili kuleta sintofahamu katika demokrasia ya nchi hii. Tusisahau kuwa nchi hii ina vyama 21 vya siasa vyenye usajili wa kudumu, hivyo basi kwanini, UKAWA wasingeshirikisha na vyama hivyo vidogo vidogo ili kudhihirisha kuwa kweli kundi la UKAWA si kwaajili ya matakwa ya vyama vya CUF, CHADEMA na NCCR-Mageuzi na kwaajili ya maslahi ya Taifa?

SASA NIREJEE KATIKA KUICHAMBUA NA KUIJIBU TAARIFA HII YA KIKUNDI CHA UKAWA.

Bila shaka kundi la UKAWA linaongozwa na wanasiasa wenye hali kubwa ya ubinadamu na watu wenye utashi mkubwa na wenye elimu zao zilizotukuka katika nyanja mbalimbali kama uchumi, sheria na hata wale wa elimu ya kidato cha nne (form IV). Kuna maswali mengi ya msingi, kama hili: Je, ni kifungu kipi cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Marekebisho yake, na Kanuni, kimevunjwa hadi sasa juu ya hasa ikihusiana na kuendelea kwa Mkutano wa Pili wa Bunge Maalumu la Katiba? Je, kuhusiana na idadi ya wajumbe wanaoruhusiwa kisheria kujadili masuala mbalimbali katika Bunge hilo imeshindwa kufikia, mpaka kusema kuwa bunge halipaswi kuendelea? Je, tukijaribu kuhusianisha SHERIA, KANUNI, TARATIBU na HEKIMA katika kuangalia mwenendo wa Bunge Maalumu la Katiba, vipi kuhusiana na kuwa baadhi ya wajumbe WAMETOKA na KUSUSIA mikutano ya BUNGE hilo kwa UTASHI NA MAAMUZI YAO? Unaposema bunge linaendelea kinyume na MATARAJIO ya WATANZANIA. Je, WATANZANIA walitegemea WAJUMBE WA VYAMA VYA CUF, CHADEMA, na NCCR-MAGEUZI kuwa siku moja wangetoka katika BUNGE MAALUMU LA KATIBA. Au Je, WATANZANIA walitarajia kuwa kungetoke kundi linalojiita UKAWA kuwa lingekuwa linawasilisha mitazamo ya WATANZANIA? Tena je, ni lini MATAKWA YA UKAWA yalijadiliwa na KUWA MATAKWA YA WATANZANIA? Je, huu si upotoshaji wa HALI YA JUU wa kujinasibisha jina la WATANZANIA huku UKAWA wakiwa na LENGO la kusukuma agenda yao ya kutamani na matamanio najisi ya MADARAKA?


Kuhusiana na UKAWA kuwa sehemu ya viongozi wa jamii, Je, kwanini iwe ni nyinyi tu (WANASIASA), vipi kuhusu sehemu nyingine ya viongozi wa jamii kama vile DINI, TAASISI ZA KIRAIA, VYAMA VYA WAKULIMA, WAVUVI NA WAFUGAJI, VIONGOZI WA WAFANYAKAZI, WANAFUNZI nk?. Wote hawa ni viongozi wa JAMII, Je, mnataka kuuambia UMMA wa WATANZANIA kuwa hawa viongozi wengine wametiwa upofu, nao wamenajisiwa kiasi cha kusindwa kuona kile kinachoendelea na kutoa maono yao CHANYA na SAWIA (ninatamani kutumia neno NEUTRAL)? Juu ya swala la kodi za wananchi, Bunge Maalum la Katiba linaendelea kuwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizolianzia, pamoja na HEKIMA, (LABDA IKIWA MTATHIBITISHA SHERIA, NA KANUNI ZIPI ZIMEVUNJWA), hivyo matumizi yanayotumika katika shughuli za kila siku za Bunge hilo ni halali, isipokuwa ikiwa kuna matumizi ambayo hajawahi kuidhinishwa na yanatumika nje ya UTARATIBU, basi TUTAHITAJI kuwajibishwa na kuwajibika kwa wahusika kwamujibu wa SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZETU.
 
Kuhusu dhana kuwa kumekosekana kwa uongozi wa kisiasa ndani ya Chama Tawala. Tunahitaji kuiangalia dhana hii kwa umakini mkubwa, kwani wengi wanaweza kushawishika kutaka kukubaliana nayo. Lakini nayo inaibua maswali mengi sana kama vile: Je, ni vigezo vipi livyotumika katika kufikia kutoa DHANA HII? Kwa mujibu wa taarifa ya UKAWA wanasema ni: 1. Mchakato unajiendea wenyewe kama vile hakuna viongozi walio madarakani 2. Viongozi wa Serikali au BMK kuwa na kauli tofauti 3. Rais Jakaya Kikwete kuendelea na 'hamsini zake' kama nchi haina tatizo lolote, mfano kumtembelea Rais Mstaafu wa Marekani G.W. Bush katika shamba lake.

Ninamesema kuwa vigezo (ASSUMPTIONS) vilivyotumika tunahitaji kuviangalia kwa makini sana kabla hatuja ingia katika mtego wa kikundi cha UKAWA, na kukubaliana nayo kama ifuatavyo:
.
MCHAKATO KUENDELEA WENYEWE KAMA VILE HAKUNA VIONGOZI MADARAKANI. Hakuna ambaye hatambui kuwa uongozi unatokana na wananchi na kuwa wananchi ndiyo wenye dhamani na nchi hii na ndiyo wanaotoa uongozi. Katika hali ya kawaida, kwa wakati huu, hadi hapo uchaguzi mkuu utakapofanyika mwakani, ni CCM ambayo imepewa dhamana ya kuendesha na kushika serikali na dola. Ikiwa MCHAKATO WA BUNGE MAALUMU LA KATIBA unaendeshwa kwa MUJIBU WA SHERIA, KANUNI, NA TARATIBU ambazo zimeliweka, huwezi kusema kuwa BMK inajiendesha tu wenyewe. Pia, kitendo cha SERIKALI kuingilia utendaji wa BUNGE hili itamaanisha kuwa MHIMILI mmoja (SERIKALI) unaingilia MHIMILI mwingine (BUNGE). JE, tukisema tufuate MATAKWA ya KUNDI la UKAWA, vipi kundi jingine likiibuka na kusema MHIMILI FULANI unaingilia UTENDAJI WA MHIMILI FULANI? Japo kuwa utaalamu wangu uko katika Teknohama na Biashara, ninautashi wa kufahamu pia kuwa THERE IS NOT ABSOLUTE SEPARATION OF POWERS AMONG THE PILLARS OF STATE. Hivyo hii haiwezi kutumia kama rungu la kuingilia mhimili mwingine na dola.
VIONGOZI WA SERIKALI au/na BMK KUWA NA KAULI TOFAUTI: Kuwa na kauli tofauti, inaweza isisikike kuuwiana na KAULI KINZANI. Japo, haijalishi viongozi wa serikali au BMK wanapishana kauli, hii inatokana demokrasia makini inayotambua utashi wa kila mtu na ni jambo la kutarajiwa, kwani haiwezekani, hata siku moja, ikatokea watu wote wakawaza, kutafakari, kuamua, na kuchagua maneno wakaati wa kutoa kauli zao kisha zikawa zinazoshabihiana. Pia waswahili husema watofautianao ndiyo wapatanao. Pamoja na kauli za viongozi hao kutokuwa za kufanana bado wameweka Umoja wa kiaifa mbele, Uzalendo mbele na Utaifa mbele. HII NDIYO SIASA SAFI. SI kama SIASA YA UKAWA YA KUSUSIA NA KULETA KERO.
RAIS KIKWETE KUENDELEA NA 'HAMSINI ZAKE'. Binafsi nimecheka sana baada ya kusoma hoja hiyo. Rais kama Mkuu wa Nchi, Kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu, alikuwa nchini Marekani, kuhudhuria mkutano wa VIONGOZI WA AFRIKA NA MAREKANI, alikuwa katika ziara ya kiserikali. Katika ziara hiyo kumtembelea Rais Mstaafu wa Marekani Bw. George W. Bush katika ranch yake, je hii inatatizo gani? Kwanini tunashindwa kuangalia uhalisia wa picha kubwa na kutumia picha ndogo kujaribu kupotosha umma. WHILE LOOKING AT THE BIG PICTURE IT IS IMPORTANT TO HOLD ON THE RELEVANT ISSUES THAN IRRELEVANT ISSUES. Bado sisemi kuwa kuonana na Rais G.W. Bushi ni jambo dogo au irrelevant, ninamaanisha kusema kuwa UKAWA wamejivisha VIATU VIKUBWA VYA WATANZANIA na VINAWAPWAYA HIVYO kuanza kutafua MASWALA ambayo hayatufikisha kuuoina msingi wa picha kubwa (KUWAPATIA WATANZANIA KATIBA MPYA NA BORA)..KWANINI WAMETOKA KATIKA MCHAKATO WA KATIBA? Kuhusiana na WATU WENGINE (MABALOZI, WAWEKEZAJI, NCHI JIRANI NA MBALI) KUENDELEA KUFUATILIA MCHAKATO, NINADHANI WANAFUATILIA KWA MAKINI SANA NA NDIYO MAANA WAMEENDELEA KUIONA TANZANIA KAMA NCHI YENYE UIMARA MKUBWA KISIANA NA KUENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA UWEKEZAJI NA KUVUTIA MITAJI MIKUBWA NCHINI.

Hivyo kuwezi kutumia hoja dhaifu, au ASSUMPTION zisizo sahihi kufika hitimisho la kusema kuendelea kwa mchakato wa kuwatafutia watanzania Katiba ni kutokana na OMBWE la uongozi. NINADHANI FIKRA SIZIZO SAHINI NA ZINAZOONGOZWA NA MALENGO BINAFSI TOFAUTI NA YA YALE YA KITAIFA ZITATAFUTA KILA JAMBO AMBALO KIMANTIKI HALITUFIKISHI KATIKA PICHA KUBWA NA KUTOA HITIMISHO LISILO SAHIHI SIKU ZOTE, KAMA AMBAYO UKAWA KWA SASA WAMEKUWA WAKIENDELEA KUFANYA.

Kuna hili neno la 'kuinajisi' Rasimu ya Pili ya Katiba Mpya nimeliona likitumika sana. Ninadhani huu ndiyo msingi wa hoja ya UKAWA katika taarifa yao. Ningependa kujikita katika hii kwa sasa.

Kama nilivyosema hapo juu kuwa Bunge Maalumu la Katiba linaendeshwa kwa Sheria, Kanuni na Tararibu zake, pia nikasema Je, UKAWA wana wezasema pasi na kuficha vifungu vilivyovunjwa vya Sheria, Kanuni na Taratibu zilitumika kuanzisha Bunge hilo? Kwa sababu katika taarifa yao kwa vyombo vya habari hawakutaja vifungu hivyo, basi mimi nitaendelea na ku-assume kuwa walipitiwa na kuwa hawakuwa na hoja ya msingi na isiyo na mashiko, kama ifuatavyo:

Ni kikinukuu sehemu ya Taarifa ya UKAWA…"…..maoni yao (Watanzania) yazingatiwe kwa kujadiliwa, kuboreshwa, na kisha kupitishwa na Bunge Maalumu la Katiba kabla wao  (Watanzania) hawajayapigia kura…." mwisho wa kunukuu. Sasa hivi UKAWA matatizo yao ni nini hasa? Ikiwa wakati wa Mikutano ya Bunge Maalumu la Katiba, Rasimu ya Pili ya Katiba imejadiliwa na…ikijadiliwa, kisha ikaonekana kuwa ina mapungufu, je, nini hutakiwa kufanyika?…wamesema katika taarifa yao (UKAWA) na mimi nikanukuu hapo juu kuwa…ijadiliwe, kuboreshwa, na kisha kupitishwa….Sasa kama imeonekana inamapungufu juu ya masuala ya ARDHI, ELIMU, MAJI, KILIMO, UVUVI, MIFUGO, SERIKALI ZA MITAA N.K. kisha mapungufu hayo yakaboreshwa kwa kuongezewa mambo hayo katika Rasimu ya Pili, je utasema kuwa yanafanyika kinyemela? Je, ni sheria, kanuni, au taratibu ipi imekiukwa katika hili, hasa mkizingatia kauli yenu kuwa BMK linatakiwa 1. KUJADILI, 2. KUBORESHA, 3. KUPITISHA..?

Hapo awali nimesema kuwa UKAWA wamevaa kiatu cha Watanzania pasipo kupata ukubali wetu (sis Watanzania), sasa kiatu hicho kimekuwa kikubwa sana. Tunajua adha ya kuvaa kiatu kikubwa, japo haifanani ya kiatu kilichobana, ila ninadhani kuwa adha ya kuvaa kiatu kikubwa kuwa ni kubwa na mbaya sana maana kila mara kiatu kitakuwa kinakutoka mguuni, ni bora ukakivua. Maana yake ni kuwa BORA ukanyamaza kimya, na kuacha kujitwisha mambo ambayo Watanzania wanafahamu nini wanachokitaka, na kuacha kuwatengenezea propaganda za uongo kuwa nchi iko katika matatizo, kumbe wewe (UKAWA) ndiye mwenye matatizo ya UROHO wa madaraka unaokusumbua.

Binafsi, siku hitaji hata kujua ni wajumbe gani wamebaki katika BMK, wanatoka chama gani au makundi gani. Binafsi, ninaangalia picha kubwa kuwa wajumbe waliobali wameonesha kuwa wao ni WAZALENDO, WAPENDA NCHI YAO, NA UMOJA  WA KITAIFA. Kuna Rais mmoja wa Marekeni aliwahisema, ninanukuu "A PERSON IS NOT FINISHED WHEN HE'S DEFEATED, BUT HE'S FINISHED WHEN HE QUITS." Ninadhani UKAWA baada ya kulikimbia BUNGE MAALUMU LA KATIBA wamekwisha, wamebaki wakitapatapa kwa kutengeneza propaganda za ajabu.

 
Mimi siyo Rais wa nchi. Siwezi kujivisha kiatu cha RAIS na kutoa maoni yangu juu ya nini afaye juu ya maamuzi ambayo UKAWA wametatoa katika tamko lao. Rais Jakaya Kikwete amepitia makubwa na madogo katika kuiongoza nchi hii tangu alipopata ridhaa ya Watanzania hapo mwaka 2005 na ameifikisha katika sehemu ambayo hata sisi tunaamini na kuliombea Taifa hili kutokana na misingi ya demokrasia, uchumi ambavyo serikali yake imeviweka na kuweha historia ya kuiongoza Tanzania kuelekea nchi ya kipato cha kati. Bila shaka utakuwa ni Rais wa mwisho kuongoza Tanzania masikini. Hivyo basi tuzidi kuliombea Taifa letu, na kuwakemea ambao wanasema kuwa eti nchi inatatizo KUBWA, TENA TATIZO LA KUTENGENEZWA NA WAO WENYEWE (UKAWA).

JONATHAN N. MNYELA
KIJANA MTANZANIA, MZALENDO.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments