Hakuna jambo linalotokea kwa bahati mbaya, bali mambo hutokea tupate kujifunza na kuelimishana. Kama una hoja tujadiliane…..
Imeandikwa kutoka katika Biblia…..
1. Na ndugu yako akikukosea enenda ukamwonye wewe na yeye peke yenu, akikusikia umempata nduguyo. La kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao liambie kanisa na asipolisikiliza kanisa pia na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru. (Mathayo 18:15-17).
Hoja
Nimekuwa nikijiuliza ni kweli Flora Mbasha alifuata hatua zote hizi na Mumewe Emmanuel Mbasha hakumsikia wala kubadilisha hatua zake mbaya mpaka ameamua kumpeleka mahakamani?
2. Kisha petro akamwendea akamwambia,Bwana ,ndugu yangu anikosee mara ngapi name nimsamehe?Je hata mara saba?Yesu akamwambia sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.(Mathayo 18:21-31). Hapa Yesu anatuambia ya kwamba hakuna idadi ambayo mtu anaweza akakukosea nawe usimsamehe, bali tunapaswa kusameheana pasipo kutazama ni mara ngapi mtu amekukosea.
Hoja
Je ni kweli Flora mbasha Amekosewa mara nyingi kiasi cha kushindwa kumsamehe Mumewe? Hapa ikumbukwe ye kwamba asiesamehe hatasamehewa, maana Mungu hutusamehe sisi pasipokujali ukubwa wa makosa yetu.
3.Lakini kwa wale waliokwisha kuoana nawaagiza ,wala hapo si mimi ila ni Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini ikiwa ameachana naye na akae asiolewe au au apatane na mumewe(waludiane) tena mume asimwache mkewe. (Wakorintho 7:10-11)
Hapa imeagizwa tena na Mungu wala sio nabii Paulo ya kwamba Mke asiachane na mumewe! Sasa ikiwa Frola Mbasha amempeleka mumewe mahakamani akimshtaki kuwa amembaka mdogoake, Je hili haliwezi kupelekea wao kuachana? Je mwanamke anayo mamlaka ya kumuacha mumewe?
Je Flora Mbasha ataweza kukaa peke yake pasipo Mume maisha yake yote yaliobaki?
4. Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. (Wakorintho 7:2)
Hapa tumeagizwa ya kwamba kila mume na awe na mke wake, kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe! Sasa huyu Flora Mbasha anataka kumfunga mume wake, je ATAPATA WAPI MUME MWINGINE? Ikumbukwe mwenye mamlaka ya kutoa tarata ni Mwanamume pia Imeandikwa Alichokiunganisha Mungu Mahakama wala Mwanadamu hawezi kukitenganisha.
5. Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. (Wakorintho 7:3)
Hoja
Je Huyu Flora Mbasha atapewa haki yake ya ndoa na nani ikiwa Emmanuel Mbasha atakaa jela miaka 30? Ikumbukwe atakapofanya tendo la ndoa nje ya mumewe AMEZINI. Je ameamua kuwa MZINIFU maisha yake yote? Maana kosa la ubakaji ni kifungo miaka 30 jela.
Ni vema kuwa makini kwa kila maamuzi tuyafanyayo,tutafakari kwa kina faida na hasara huku tukikumbuka ya kwamba kila mtu anastahili kusamehewa pasipo kutazama ukubwa wa kosa lake.....
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments