Katika kile tunachoita "Umoja ni nguvu" kama tunavyoona kwenye suala la katiba, basi kama kweli nia yenu ni kuhakikisha watanzania wanafanya mabadiliko ya kweli na kupata katiba itakayokuwa imetokana na watanzania wenyewe, basi hamna budi ya kuiendeleza hii "UKAWA" hadi kwenye UCHAGUZI MKUU 2015.
Nikijaribu kuangalia, ni jinsi gani upinzani utaweza kuiondoa CCM madarakani katika uchaguzi mkuu kiurahisi zaidi, ni kuwa na "UKAWA" ya kuipeleka nchi kuvuka 2015 salama kabisa huku mkiondoa ile dhana ya kuwa Tanzania ni Nchi ya CCM tu. Kuibuka kwa vyama vingi nchini, ni strategy ya kufanya CCM iendelee kutawala milele, kwamaana wale wanachama watakuwa wanagawanyika nao bila kuwa kitu kimoja. Naamini ninyi UKAWA mkiamua kutengeneza UKAWA ya kuivusha tanzania kwenye 2015 General Election (GE) mtaibuka na ushindi mkubwa sana! We need changes, with vision ya kuifanya Tanzania iwe mahali ambapo mwananchi wa kawaida anajua faida ya rasilimali zake, anajua jasho lake linavyotumika katika kumletea maendeleo, nk.
Katiba haikuwa kwenye Ilani ya Chama tawala, kwa maana kwamba hakikuona kama Katiba inahitaji marekebisho au tunahitaji kupata katiba mpya. Wapinzani ndio mmliona hilo kuwa katiba mpya italeta mwanga katika nchi yetu. Kama mnaona Bunge maalum halina mpango wa kuleta katiba mpya? Basi endelezeni UKAWA huo ili mje kuleta katiba mnayoona itakuwa kweli imetokana na wananchi.
Mimi nitaona kuwa kweli mnaipenda Tanzania kama UKAWA ya uchaguzi mkuu 2015 itaibuka tena na kuwa na misimamo kama hii ninayoiona sasa. Najua viongozi, wanachama na wapenzi wa UKAWA mpo hapa jukwaani, tunataka ukawa ya 2015 kuiondoa CCM madarakani.
--
Ipyana LwingaEmail: ipyanalwinga@gmail.com
"Mpende Jirani yako kama nafsi yako..."
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments