MATALA
Duh sijui ni kikabila gani wanaita hivyo haya twende
Allah aliruhusu wake mwisho wanne kwa sababu maalumu sio mnavyofanya waume zetu wa leo mweee!!!
Enyi wanaume muwe mnajua na sisi tuna mioyo na tunaumia sana msituone kuvumilia.
nimeanza na hasira eeh
Ewe mume uliyeoa kwa mapenzi yako tena ukiwa katika hali duni ya kimaisha, mke akavumilia kushinda njaa, kuvaa kauka nikuvae, kuchekwa na kudhihakiwa mtaani nawe unampa maneno mazuri ya subira tena unamsisitiza akuombee dua ipo siku nae atakuwa na hadhi.
Mungu mkarimu anawapa kiasi cha kubadili mboga KOSA!!!
Mume unakuwa kama umerogwa uchizi ndio sasa utaanza kumuona huyu mwanamke hafai sio hadhi yako tena.
mbio unaenda kuoa na kumleta mke mwingine kwa vishindo tena ushamjaza maneno ya uongo kuwa mkeo ana roho mbaya, mchafu, hajui kupika, unakaa naye kwa sababu ya watoto jamani nyie wanaume nyie baadhi yenu Mungu atawachoma wallahi!!!
Haya nawe bi mdogo ndio utayabeba na kuja mfanyia visa mke mwenzio bila kutakafari na kujua wapi walikotoka.
Bi mkubwa masikini akisema hasikilizwi na mume anakuwa kama kishada. Mke ametoka katika kwenye mateso ya hali duni anaingia kwenye manyanyaso kwa mali aliyoshiriki kuichuma, mwisho yanamshinda anaamua kuondoka anaacha watoto wake anawapenda, na basi utawanyanyasa hao watoto mpaka wamfuate mama yao.
Na we mume kimya ushapewa inama nikuchume familia inaharibika husikii wala huoni.
nyie waume baadhi yenu ndio mnafanya wanawake wachukie ukewenza maana ni mateso.
Ndio mnazalisha Umasikini, ukosefu wa elimu, watoto wenye mazingira magumu, n.k
MUOGOPENI ALLAH JAMANI NA SIE NI VIUMBE KAMA NYIE.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments