Nimekusikiliza ukichangia budget ya mambo ya ndani, mwanzoni nilikuelewa uliposisitiza umuhimu wa viongozi hasa wa kisiasa kutoa matamko yanayo wagawa wananchi hasa kuwagawa kidini,ulichonichanganya ni pale ulipo sema serikali inakosea kuongea na BAKWATA kwani sio chombo kinachokubalika na waislamu wote,inawezekana ni kweli kutokana na utafiti wako lakini pengine unguzitaja taasisi nyingine zilizo omba kuongea na serikali sikakataliwa na ni kwa masuala yapi kwani kama sijakosea nadhani ni serikali hiyohiyo iliyoongea na waislamu ambao sio BAKWATA na kuwapa chuo cha TANESCO kama sija kosea na kuwa chuo cha kiislamu Tanzania.Mimi nadhani ungetoa mfano wa tasisi hizo badala ya kuitaja BAKWATA kutokubalika na kuacha kutaja taasisi nyingine zilizonyimwa haki hiyo ya kuongea na serikali.Vilevile unaposema serikali isijihusishe na masuala ya kidini hukufafanua najua muda wa dakika tano hautoshi lakini nivizuri ukawaeleza watanzania kujihusisha kivipi ili tupate tafsiri sahihi.Mimi binafsi serkali kusaidia taasisi ya kidini kama ya kiislamu kupata eneo la kutoa huduma za kijamii kama elimu(Chuo cha kiislamu ni sahihi) lakini kwa uendeshaji dini pengine inaweza isiwe sahihi.Nahisi badala ya kusaidia kutatua tatizo wewe ndio unamwaga petroli Mh tueleze hata muamsho na vikundi vingine vya kigaidi navyo vipewe nafasi mimi binafsi nadhani sio sahihi,Mwisho tuambie grievancies unazotaka serikali kushughulikia nizipi au ni zile tunazosikia kila siku kwenye mihadhara?
Related Posts
- [wanabidii] AN EXPERIENCED PROFESSIONAL DRIVER LOOKING FOR A JOB
- [wanabidii] A VERY EXPERIENCED BUSINESS ADMINISTRATOR CUM ACCOUNTANT LOOKING FOR A JOB
- [wanabidii] Press Releases: "Showcasing the Bioeconomy: The Future is Now" Biotechnology Conference
- [wanabidii] WATENDAJI DAR WAASWA KUSHIRIKIANA ILI KUWEKA JIJI KATIKA HALI YA USAFI
- [wanabidii] AN EXPERIENCED FEMALE HOTELIER LOOKING FOR A JOB
- [wanabidii] Maisha ya 'Geto' Changamoto kwa Wanafunzi Sekondari za Kata Tanga
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments