[wanabidii] TAMKO LA MWANAKIGOMA KUHUSU MGOGORO CDM

Friday, November 29, 2013
Naendelea na maombi kanisani kuwaombe "busara" viongozi wa chadema
makao makuu a waliovuliwa madaraka bila kuwasahau wanachama wa kwlei
na uongo waliopata kuchangia suala hili tangu lilipoibuka

naanza.......
najua yeyote mwenye busara katika hili ambaye hana chuki yeyote wala
maslahi binafsi kati ya pande hizi mbili

basi hawezi kutoa msimamo wowote unaolenga kumchafua kiongozi aliye
ndani au vuliwa madaraka naona kama hiyo nikivuruga zaidi

jamani haya yametokea kama unadhani huna uchungu na namna chama
kinavyoharibiwa kwa tukio hili basi kaa kimya si lazima uchangie au
utoe msimamo nakuwaaminisha watanzania unavyodhani

tambueni kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi

nadhani busara zitimike kumaliza mgogoro huu bila kuwakumbusha watu na
kuwakalilisha kuhusu udini, ukabila na ukanda vyote hivyo vinafaanya
watu wachukie zaidi chadema ambao tunaona wananchi wengi wanekuwa
wakiamini zaidi katika upinzani.

mambo hayo mnayasema mnaojiita viongoxi vipi katika vikao vya chaka
mmewahi kusema?

kumbikeni nyie viongozi mliapa kuoinda na kutetea chama lakini leo
mmoja anamwaga mbonga mwingine ugali then pande zote mnaona sifa
kuweka hadharani uozo wenu kwani vikao vyenu mlivituiaje?

someni vizuri tahariri ya gazeti la Jamuhuri siku chache zilizopita
tutapata chadema yenye nguvu

Mbowe ni nani! Dk Slaa na Zitto ni nani chadema hawa ni zaidi ya chama?

shida ya viongoxi kuwa na sifa zaidi ya chama ndio hivo hawa watimie
busara ikishindikana wajiuzuru tupate wengine.

tusishindwe kuendesha chama kwa hofu ya kuitwa udini, ukabila,
misimamo, ukanda, nani na wa dini gani alinyimwa fomu kwakuwa ni dini
fulani au mkoa fulani?

hao waliofukuzwa arusha niwa ukanda wa wapi? mbeya au Tabora?
jamani hivi mwenyekiti, katibu mkuu au naibu wake ni nani katika vyama?

kama wajumbe wanapinga jambo kwa wingi viongozi hawa wana mamlaka kwa
nyadhifa zao kupinga? basi wajumbe wanakuwa dhaifu na wajiuzuru kwani
wanaburuzwa na hawafai.

kama vipi wanachamavwenzangu hawa watu hawatufai kwann wao lazima
kugombea? kwani Zitto aliyetumia nguvu nyingi kujenga chama anaona
fahari chama kife kwa sababu binfsi za uenyekiti tena wakati huu wa
kushika dola

kwani Mbowe ameambiwa bila yeye kuendelea kuwa chair chadema haiwi hai?

tunawapa vichwa sana watu hawa nadhani chadema ni taasisi kubwa kuliko hawa

"sisi wanachama tutakuwa wajinga kukimbatia watu hao kwa maslahi yao
binafsi kana kwamba bila wao hakifanyiki kitu, je! wakifa leo chadema
inakufa?"

viongoxi wilayani mikoani ni ujinga kubwa kudhani matsmko yenu kuuga
au kutounga mkono maamuzi ya kamati kuu kuwa yanasaidia chama ni kuuwa

wito cdm makao makuuvangalieni jambo hili kama kuma chuki na fitna
mjiuzuru au malizeni kwa vikao vya muafaka na kwa makubakiano maalimu
ili atakayekiuka basi aadhibiwe

naomba kamati kuu na waliofukuzwa acheni kutunishiana misuri ni aibu
kwenu na chama kwani mwehu akichukua nguo zaki bafuni wwkati unaoga
busara nikumkimbixa ukiwa uchi au unatilia kungoja ndugu jamaa na
marafiki wakuletee nguo ujisitili kisha ufuatilie nguo hizo au uache?

mwisho, huu ni mtihani kwenu kadri mtakavyo limaliza bila
kusambaratisha chama ndivyo tutakavyokuwa na imani na nyie katika
kuelekea kuongoza nchi

tahadhari, hapa ndipo tutamjua anayetumika kuuwa chama kuelekea
uchaguzi mkuu 2015 kati ya makundi hayo

chonde chonde acheni kutumia vibaya media kujidharirisha kwa hayo
tumieni vikao rasmi na visivyo rasmi mmalize

wasalaaam, Mungu ibariki Tanzania ibariki CDM, Amini!!!!!!

Jacob Ruvilo,
mwanachama, kigoma
0787265298

On 11/29/13, Chadema Tanga <mabadilikochadema@gmail.com> wrote:
> *TAMKO LA MJUMBE WA BARAZA KUU , MKUTANO MKUU CHADEMA, MJUMBE WA KAMATI
> TENDAJI YA BARAZA LA VIJANA TAIFA (BAVICHA), MWENYEKITI WA VIJANA MKOA WA
> TEMEKE NA MWENYEKITI WA CHADEMA JIMBO/WILAYA YA TEMEKE KUHUSU MGOGORO NDANI
>
> YA CHAMA NA UAMUZI WA KAMATI KUU KUWAVUA NYADHIFA MJUMBE WA KAMATI KUU
> Dkt. Kitila Mkumbo na NAIBU KATIBU MKUU zitto kabwe *.
> *UTANGULIZI. *
> Mimi Patrick Y.Joseph, ni mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na
>
> maendeleo CHADEMA ninayeshikilia nyadhifa mbali mbali kwa sasa kama
> inavyoonekana hapo juu kwenye kichwa cha Habari. Ninawashukuru kujitokeza
> kwenu hapa ili tushirikiane kuufikisha ujumbe kwa Watanzania kuhusiana na
> maswala yanayoendelea kwenye chama chetu hivi sasa.
>
> *MIGOGORO NDANI YA CHAMA*
> Chama chetu kimekuwa na tabia ya kuingia kwenye migogoro kila panapokaribia
>
> chaguzi mbali mbali za ndani ya chama, migogoro hii hupelekea mpaka
> kuchafuana na kutukanana miongoni mwetu kiasi cha kuitana wahaini, wasaliti
>
> na wengine kuwaita wenzao wanatumika lengo likiwa ni kuwadhoofisha mbele ya
>
> wanachama na jamii kwa ujumla.
>
> Tumeiona mifano mingi ya namna hii, wakati marehemu Chacha Zakayo Wangwe
> alipotangaza kugombea uenyekiti mgogoro wa namna hii ulijitokeza, aliitwa
> majina yote mpaka anapoteza uhai wake hakuwa akisemwa vizuri kwenye chama,
> hakuchafuliwa na watu walio nje ya chama. Alichafuliwa na viongozi wenzie
> waliotofautiana msimamo.
>
> Alipotangaza zitto kabwe kugombea uenyekiti hali ikawa hiyo hiyo, akaitwa
> msaliti, anatumika na mengineyo mengi, alipotangaza kujitoa kugombea
> akaachwa kidogo apumzike.
>
> Tunakumbuka yaliyotokea wakati wa chaguzi za ubunge wa viti maalum,
> tunakumbuka pia chaguzi za mabaraza ya chama, wakati nagombea nafasi ya
> umakamo mwenyekiti wa vijana nako pia waliogombea uenyekiti waliitwa kila
> aina ya majina.
>
> Kwa kifupi migogoro hii ni ya kutengenezwa ili kudhoofishana kuelekea
> chaguzi za ndani ya chama.
> Hivi sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa chama tumeshuhudia tena
> Zitto Kabwe na Dkt Kitila Mkumbo wakikutana na dhahama hiyo hiyo.
>
> Hali hii si nzuri kuruhusu iendelee kushamiri ndani ya chama maana
> haikijengi chama zaidi ya yote inakibomoa tu.
>
>
>
> *KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU*
> Nikiwa kama mjumbe wa Baraza Kuu la chama ninayewakilisha wilaya ya Temeke,
>
> na nikiwa kama mjumbe wa Kamati Tendaji ya Baraza la vijana la Taifa (
> *BAVICHA)*
>
> Nimefadhahishwa sana na uamuzi uliofikiwa na kamati kuu ya chama dhidi ya
> ndugu Zitto kabwe na Dkt. Kitila mkumbo.
> Ukiachilia mbali kwamba kamati kuu haikuwa na mamlaka ya kikanuni wala
> kikatiba kufikia maamuzi iliyoyafikia na kuyatangaza kwa umma.
>
> Lakini imeonyesha ni jinsi gani wametawaliwa na Chuki, Ghadhabu, Unafiki na
>
> Ubaguzi uliopitiliza.
>
> Ni uamuzi ambao hauwezi kuungwa mkono na mwanachama yeyote mwenye akili
> timamu,kwa kuwa haukisaidii chama badala yake unapandikiza chuki miongoni
> mwa wanachama.
> Uamuzi huu uliojawa na hofu kubwa ya kiuchaguzi, hofu ya madaraka na hofu
> ya kupoteza umarufu unapaswa kukemewa na kusababisha watu wenye akili
> timamu wajiulize mara mbili mbili kama ni sawa ama la.
>
> Kwa mantiki hiyo basi, nikiwa kama mjumbe wa baraza kuu, ninatoa masikitiko
>
> yangu kwa kamati kuu kufanya kazi isiyowahusu tena bila kufuata hata kanuni
>
> wala Taratibu zozote za kinidhamu baina ya viongozi.
>
> Ningependa umma utambue kuwa sikubaliani na uamuzi huu kwa kuwa haukidhi
> misingi ya kidemokrasia wala kufuata utawala wa sheria.
>
> Haiingii akilini hata kidogo kwa chama kinachopanga mikakati mbali mbli ya
> kuhinda dola, kuwafukuza na kuwaogopa watu wanaopanga mikakati ya wao
> kushinda uchaguzi ndani ya chama.
>
> Kama ni kweli kupanga mikakati ya uchaguzi ndani ya chama ni uhaini na
> usaliti, basi Operesheni zetu za chama ikiwemo M4C zenyewe zinapaswa kuwa
> uhaini uliopitiliza kwa kuwa nazo ni mikakati ya chama kushika dola.
>
>
> *MSIMAMO WANGU*.
>
> Ninamtaka mwenyekiti akishirikiana na watendaji wengine wa chama waitishe
> mkutano wa dharura wa baraza kuu ili tutolee maamuzi sahihi swala hili.
>
> Ninataka pia pamoja na agenda zitakazojadiliwa,
> *(i).* *watueleze ni kwanini wameamua kusambaza waraka wanaozani
> unawadharirisha kina zitto na mkumbo badala yake waraka huo unakidharirisha
>
> chama kwa kuonyesha madhaifu ya mwenyekiti na katibu mkuu wa chama*.
>
> *(ii). Ni kwanini tusiamini kwamba maamuzi haya yameathiriwa na hofu ya
> chaguzi za ndani ya chama* .
>
> *(iii). Ni kitu gani kimeifanya sekretarieti ya kamati kuu itangaze ratiba
> ya uchaguzi mkuu wa ndani ya chama baada ya kuwachafua miongoni mwa watu
> waliotarajiwa kugombea nafasi mbali mbali mpaka kuwavua uanachama*.
>
> Ni vema sasa tu tukijenge chama chetu bila kufuata maswala ya ubaguzi wa
> kidini na kikabila ama kikanda.
>
> Chama chetu kimekuwa kikishtakiwa sana kuhusiana na matatizo ya kidini na
> kikabila, lakini pia chama chetu kimekuwa kikiwatumia Zitto na Arfi kama
> ishara ya kutokuwa na udini ndani ya chama, sasa inawezekanaje kuwatimua na
>
> kuwaita wasaliti watu ambao mmekuwa mkijivunia.
>
>
>
> Mwisho ninapenda kusema kuwa huu ni msimamo wangu na kwamba sipo tayari
> kuburuzwa wala kuruhusu kuona tunaendelea kuibomoa demokrasia
> tunayoitangaza kila kukicha.
>
> Nitaendelea kuwa mwanachama mtiifu wa chama changu, na kukishauri namna
> bora ya kuendeleza demokrasia ndani ya vikao na sita ogopa kueleza maoni
> yangu kwa Watanzania.
>
> Nawashukuru sana.
>
> Imetolewa na ;-
>
> *Joseph* *Y.*
> *Patrick*
>
> +255713802226
>
>
> Mwenyekiti wa chadema wilaya/jimbo Temeke
> Mwenyekiti BAVICHA mkoa wa Temeke
> Mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa
> Mjumbe wa mkutano mkuu wa Chadema Taifa
>
> --
> Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
>
> Kujiondoa Tuma Email kwenda
> wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha
> ukishatuma
>
> Disclaimer:
> Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal
> consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be
> presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to
> this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
> ---
> You received this message because you are subscribed to the Google Groups
> "Wanabidii" group.
> To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an
> email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
> For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
>

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments