[wanabidii] Sera Ya Gesi

Friday, November 29, 2013
Ndugu Wanabidii,

Nimemsoma Reginald Mengi akisemea kupitia gazeti la Mwananchi la leo kuhusu sera ya Gesi. Mimi binafsi ninakiri kuwa anachosema kuhusu ushirikishwaji wa wananchi kina maana. Je Sera ya Gesi iliyozinduliwa hivi karibuni ina manufaa kwa Wazalendo kama ndio kwa vipi kama sivyo kwa vipi? Je tunahitaji Sera mbadala ambayo itaeleza bayana kwamba wananchi watashiriki kwenye shughuli za gesi kuanzia utafutaji, na uchimbaji, usafirishaji, uhifadhi na uuzaji jumla?

Naomba michango yenu ili tuweze kujenga hoja kwa Serikali yetu ambayo tunaamini ni sikivu.

Ahsante


Herment A. Mrema

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments