[wanabidii] Makubwa Ya Mwaka 1995: Kwenye Furaha Ya Mwalimu Kwa Ushindi Wa Mwanawe Makongoro ( NCCR-Mageuzi) Kulikuwa Na Huzuni Ndani Yake..Kwanini?

Thursday, January 08, 2015


Ndugu zangu,

Nimekuwa nikisimulia matukio ya mwaka 1995 yenye lengo la kuamsha pia mijadala. Jana nimezungumzia kisa cha mwana wa Mwalimu, Makongoro Nyerere aliyehama CCM mwaka 1995 na kuhamia NCCR Mageuzi ya Mrema. Makongoro akashinda jimbo la Arusha Mjini.

Kwenye moja ya mahojiano yake na wanahabarri, Mwalimu Nyerere alipata kutamka, kuwa moja ya siku za furaha maishani mwake ni siku ile alipopata habari kuwa mwanawe makongoro Nyerere ameshinda kiti cha Ubunge arusha mjini kwa tiketi ya NCCR Mageuzi ya Augustine Mrema.

Hata hivyo, tuliokuwa tukifuatilia kauli na maandiko ya Mwalimu kuelekea 1995 tunafahamu, kuwa Mwalimu hakuwa na furaha na yaliyokuwa yakitokea ndani ya CCM. Nyerere na WanaCCM wengi walianza kutoitambua CCM yao. Kwamba chama kilianza kupoteza mwelekeo.

Na vuguvugu la mabadiliko miaka ile ya CCM lilikuja katika wakati hasa ambpo demokrasia ndani na nje ya CCM ilizidi kusiginywa. Wakati ambapo rushwa ilianza kutamalaki. Kwamba dalili na vitendo vya wana CCM kununua uongozi zilianza kuwa wazi.

Kipindi hicho, Mwalimu alionekana kuwa mwenye kutatizwa na CCM kutokujitambua. Mwalimu was in search for the soul of his Party. Nimeazima maneno ya Kiingereza, nikiwa na maana Mwalimu alikuwa akiutafuta Moyo wa Chama chake. Yumkini, Mwalimu alikuwa akiweka mazingira ya ' Uasi wa Kiitikadi' ili wanaCCM wengine waingie kwenye kazi hiyo ya kuutafuta moyo wa Chama.

CCM imshukuru Mwalimu kwa kuanzisha kazi ile, kuweka mazingira ya kuwa Si Dhambi kuishutumu CCM ukiwa mwana ccm. Ndio matokeo ya misemo ya ' CCM si baba wala mama yangu'. Misemmo ya ' Upinzani wa Kweli Utatoka Ndani ya CCM'.

Mwalimu alikuwa sahihi. Na matokeo tumeanza kuyaona.

Maggid Mjengwa.
Iringa.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments