UDHAIFU WA HOJA YA UFISADI WA RICHMOND DHIDI YA LOWASSA
Lowassa Ni Sawa Na Askari Mtiifu Kwa Nchi Yake Na Chama Chake Anayetoa Uhai Wake Kwa Ajiri Ya Utulivu Na Mustakabali Wa Nchi Yake.
Na Ndio Maana Hata Msingi Wakujihudhuru Kwake Ulikuwa Katika Kutekeleza Dhana Ya Kiungwana Na Kizalendo Ya Uwajibikaji, Kulinda Maslai Mapana Ya Serikali Na Chama Chetu Cha Mapinduzi Kupitia Dhana Ya Uwajibikaji.
Ikumbukwe Kuwa Mchakato Wa kumpata Mkandarasi Wa Kutupatia Umeme Wa Dharula Kutokana Na Tishio La Nchi Kuingia Gizani Ulipitia Kwenye Baraza La Mawaziri Chini Ya Mwenyekiti Wake Na Kupata Baraka Zote Na Baraza Lenyewe Lakini Pia Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mawaziri.
Baraza Lilitambuwa Kwamba Edward Lowassa Alipeleka Katika Baraza Maoni Na Ushauri Kitaalamu Alioupokea Kutoka Kwa Watendaji Wa Wizara, Baraza Halikuwa Na Shaka Kabisa Na Edward Likitambua kuwa Lowassa ni mchapa kazi Asiyependa Kuona Nchi Inaingia Katika Taharuki Ya Kukosa Huduma Muhimu Inayoweza Kukwamisha Masuala Mtambuka Kukwama,
Ofisi Yake Ikabeba Jahazi Akapewa zoezi La kufuatilia Kwa Uharaka Upatikanaji Wa Mkandarasi Huyo Yeye Akiwa Kama Kiranja Mkuu Wa Usimamizi Wa Serikali Na Maazimio Ya Baraza La Mawaziri Haswa Ukizingatia Mchakato Huu Ulipitia katika Njia Za Kitaalam kwa Kupata Ushauri Na Baraka Zote Za Baraza La Wataalamu Kwa Maana Ya Makatibu Wakuu Kama Washauri Na Barua Ya Mawaziri Kama Ushaidi Wa Kili Kinachofanyika Kuwa Ni Sahihi,Go Ahead Kutoka Kwa Mwanasheria Mkuu Wa Serekali Inaonyesha Dhahiri Katika Mchakato Huu Hakukuwa Na Ubabaishaji Kutoka Kwa Lowassa Bali Wataalamu Na Makatibu Wa Wizara
Utaratibu Uliopitia Unaweka Wazi Sura Ya Kuwa Serikali Yote Ilishiriki Na Kufanya Maamuzi Juu Ya Mchakato Wa Kandarasi Ya Umeme Wa Dharula Na Kufikia Maamuzi Juu Ya kuipa kandarasi hiyo kampuni ya Richmond Hivyo Lowassa Kama Kiranja Mkuu Alisimamia Maamuzi Ya Baraza Na Si Yake Wala Ya Familia Yake.
Ikumbukwe Mara Kadhaa Lowassa Alitia Mashaka Juu Ya kampuni Hii Na kutaka Kughairisha Mkataba Na Kampuni Hii Lakini Mamlaka Zilizokuwa Juu Yake Zilimsihi Kuendelea Na Maelekezo Aliyopewa Kama Kiranja Mkuu.
Kilichomponza Lowassa Ni Dhana Yake Ya Utiifu Kwa Mamlaka Za Juu Yake Alitekeleza Kwa Hekima kile Alichoshauriwa Kufanya Na Hapo Ndiyo Tukaipata RICHMOND ILIYOSABIBISHA AJARI YA KISIASA KWA MPENDWA WETU.
Yapo Mambo Ya Kujiuliza ;
1.Sasa Kama Mchakato Ulipitia Kwenye Baraza La Mawaziri Na Kuridhiwa Na Wajumbe Wake Pamoja na Mwenyekiti Wa kikao Hicho Na Kupata Ushauri Wa Baraza La Wataalamu Yaani Makatibu Wakuu Iweje Sasa AWAJIBISHWE LOWASA PEKE YAKE......?
Na Hapo Sasa Tunaweza Kurejea Hotuba Yake Kuwa ISSUE NI UWAZIRI MKUU Ndio Uliokuwa Ukitafutwa Na Wala Siyo Kitu Kingine.
2.Baada Ya Tuhuma Ya Richmond Tume Ya Uchunzi Chini Ya Mwenyekiti Ilishindwaje Kufuata Msingi Wa Haki (Natura Justice) Kumhoji Na Kumsikiliza Mtuhumiwa......?
Hapa Inaonyesha Zairi Issue Ya Richomnd Ilikuwa Ni Ya Kupikwa Na Ndio Maana Tume Ilihoji Watu Wote Mpaka Nje Ya Nchi Kasoro Mtuhumiwa No Moja.
3. SASA Baada ya Lowasa Kujihudhuru Je Richmond ilifukuzwa Au Bado Ina Peta Tu na kama ipo kwa nini?
Utaona Mwendelezo Wa Mpango Wa Watu Waliokuwa Wakimtengenezea Sakata La Richomond Lowassa Kuendelea Kuaibika.
Richmond Hata Baada Ya Kujihudhuru kKongozi Mahiri Bwaana Lowassa Bado Iliendelea Kuwepo kwa Baraka Zote Hadi Za Wale Waliomdhikaki Lowassa Ingawa Ilijibadili Rangi Yake Kuwa Dowans Na Kuendelea Kuufanya Kazi Zake Na Hatimaye Baadae kubatizwa Upya Jina La SYMBION Na Hapo Ndipo Tulipo Ishuhudia Dunia Nzima Ikiambiwa Symbioni Ni Kampuni Bora Ya Umeme Na Itakayoweza Kuwasaidia Watanzania.
Tukashuhudia balabala zikidekiwa ubungo na jiji lote kuwa safi kama Eden kwa ujio wa Obama na tukashuhudia Viongozi Wetu Wakiisifia Symbioni Pale Ubungo Na Hata Kucheza Mpira Wa Kama Ishara Ya Kuwapongezana kwa Mafanikio Ya Uwekezaji Wa Symbioni=Dowans=Richmond.
Sasa Tujiulize Symbion Ni kampuni Ya Kimarekani Iliyonunua Mitambo Hiyo Toka Kwa Dowans Na Kwa Level Yao Ya Ujasusi Ilivyo Kama Kampuni Hii Ingekuwa Ni MAGUMASHI je wangekubali Kumleta Raisi Wao Pale Ubungo ????
Mwisho Tujiulize Tangu Lowassa Kajihudhuru Ni Kashifa Ngapi Za kifisadi Zimeikumba Serikali Yetu Na je Zimemhusisha Lowassa...?
Watanzania Wanajua Lowassa Hakuusika Na Richomond Aliwajibika Kisiasa, Watanzania Wanajua Licha Ya Kutokuhusika Hakuna Hata Cent Moja Ya Kitanzania Ilioingia Katika Mfuko Wa Lowassa, Watanzania Wanajua Ulikuwa Ni Mpango Wa Kumuondolea Uhalali Kisiasa,Heshima Edward Lowassa Mbele Ya Umma.
May 5, Historia Itaandikwa Upya Ni Siku Ya Ukombozi Wa Fikra Na Matumaini Mapya Kwa Nguvu Ya Maamuzi.
Kutoka
Kwa Mpiganaji Ukombozi Wa Fikra
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments