[wanabidii] Uraia pacha dhana yake ikoje?

Friday, August 15, 2014
Umekuwapo mjadala wa Tanzania kuruhusu uraia wa nchi mbili na hawa Tanzania wanaoishi nje ya nchi naamini ndo wanufaika na mchakato huu wamekutana dar kujaribu kusukuma hoja hii. Nasikia wakiruhusiwa uraia wa nchi mbili watasukuma maendeleo na uchumi wa nchi kwa kuleta fedha na mitaji waliyochuma huko nje.

Lakini nimeona watanzania kama al-aldawi (dowan) wakiwekeza na badae kuamua kutimua. Sasa sijui labda uraia wake wa oman ulikuwa tatizo au?

Limekuwepo tatizo la kodi, miaka ya tisini vijana hawa waliingiza magari ya ulaya kama vogue lombardin na mercides benz, tangu tra waje na utaratibu mpya wa kukokotoa kodi, haya mavogue hayaji tena.

Lipo tatizo la machotara waliozaliwa na wabongo hujo nje wakitaka kuja wanakuja kama watalii na kulipia visa na kutakiwa kuondoka baada ya visa kuisha muda.

Je katiba mpya inaweza kuwa suluhisho ya tatizo hili? Je kuna tija kuruhusu utaratibu huu?

----------
Sent from my Nokia phone

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments