-------- Original Message --------
Subject: [wanabidii] BUNGE MAALUM LA KATIBA; TUMETOKA WAPI, TUKO WAPI NA TUNAKWENDA WAPI
From: Yona Maro <oldmoshi@gmail.com>
To: wanabidii <wanabidii@googlegroups.com>,Wanazuoni <wanazuoni@yahoogroups.com>
CC:
Na Julius S. Mtatiro
BUNGE MAALUM LA KATIBA; TUMETOKA WAPI, TUKO WAPI NA TUNAKWENDA WAPI.
1. Wajumbe wengi(asilimia 81) kati ya wale 201 walioteuliwa na Rais Kikwete
ni viongozi na wanachama waandamizi wa CCM. Tukavumilia na kukaa kimya.
2. Kwenye kutengeneza kanuni za Bunge Maalum CCM walipambana kila kukicha
kupitisha kanuni zitakazotetea MFUMO wao - tukatumia nguvu kubwa kuwazuia
lakini tulifanikiwa kidogo sana -Tukakaa kimya.
3. Katika kuanza kuzitumia kanuni, Mwenyekiti wa Bunge Maalum kwa shinikizo
la wazi la CCM alikiuka kanuni bila aibu, ikapangwa kuwa hotuba ya Jaji
Warioba ianze ili aje Rais wa nchi baadaye, jambo hili ni kinyume kabisa na
kanuni. Suala hili likaleta mvutano mkubwa sana tukaamua KUJIFANYA HATUTAKI
MAKUU, tukaliacha - Tukakaa kimya.
4. Jambo hili lilipokubalika, CCM wakamshinikiza Mwenyekiti wa Bunge Maalum
amnyime jaji Warioba muda. Mwenyekiti akatangaza kuwa atampa dkk 60 tu,
tukakataa, siku jaji Warioba alipokuja kuwasilisha tukalikwamisha ili
aongezewe muda, baada ya mashauriano ya baadaye, ikakubaliwa apewe saa nne.
5. Baada ya uwasilishaji wa Rasimu wa Warioba, Rais Kikwete alikuja na
kuivunjavunja na kuweka misimamo ya chama chake dhidi ya maoni ya wananchi
yaliyomo kwenye rasimu ya katiba. Tukamsikiliza Rais kwa nidhamu kubwa na
kuvumilia hatua yake ya juu ya kupinga hadharani rasimu ya katiba ambayo
imetokana na maoni ya wananchi ambayo ameyakusanya baada ya kuiunda tume ya
Warioba. Tukakaa kimya.
6. Ikumbukwe kuwa hata kwenye kuchagua Mwenyekiti wa Bunge la Katiba CCM
walipigania nafasi hiyo na kushinda. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti pia
waliipigania wakachukua. Tukakaa Kimya.
7. Jana Mwenyekiti wa Bunge la Katiba aliteua kamati za uandishi na kamati
ya Kanuni. Kamati zote hizi mbili, kila moja, mwenyekiti na makamu
mwenyekiti walioteuliwa wote ni viongozi wa CCM, Tukakaa kimya. Wenyeviti
wa kamati hizi wote wanaingia kwenye kamati ya uongozi ya Bunge Maalum.
Tumekaa kimya.
8. Juzi CCM walipokutana kwenye kikao cha wajumbe wa CCM waliamua kuteka
kamat zote 12 zitakazojadili sura za Rasimu ya Katiba.
Jana tulipokwenda kwenye uchaguzi wa viongozi wa kamati, wateuliwa wote wa
CCM walishinda akiwemo HAMAD RASHID na Dr. Francis Michael ambao pia
wamejivika joho la kusimamia maoni ya wananchi huku ukweli halisi ni kuwa
wapo ili kusmamia matwaka na Maslahi ya CCM.
Ikumbukwe kuwa, wenyeviti wa kamati hizi 12, wote ni wajumbe wa kamati ya
Uongozi ambayo ndiyo dira itakayoongoza kila jambo linaloletwa katika bunge
Maalum.
9. Leo, Mwenyekiti wa Bunge Maalum ameteua wajumbe watano ili kuingia
kwenye kamati ya uongozi kama kanuni zinavyoelekeza. Jambo la ajabu ni
kuwa, kati ya nafasi hizo 5, nafasi 4 zote amewateua wajumbe ambao ni
viongozi waandamizi wa CCM akiwemo mwakilishi wa walemavu Amon Mpanju.
Mjumbe mmoja wa walemavu amesimama na kupinga uteuzi wa mwakilishi wao
palepale.
Prof Lipumba amesimama na kukataa uteuzi huo, ameeleza si wa haki hata
kidogo. Ameeleza alijiunga na siasa ili kutafuta haki za wananchi na umoja
wa kitaifa na si vinginevyo. Lipumba amesema kuwa hawezi kutumika kama
mhuri.
Kama CCM wana nia njema wasingehodhi nafasi zote katika mchakato wa katiba.
10. Hoja kubwa ya CCM kuchukua nafasi zote za uongozi wa bunge maalum ni
"eti" wao ni wengi. Hoja ya ajabu sana hii! Kama hoja ni nani au kundi gani
lina idadi gani basi nafasi hizi zingegawanwa kwa mantiki hiyo. Vyama
visivyo CCM peke yake vina wajumbe zaidi ya 130, kama hoja ni wingi vyama
hivi peke yake vingepewa nafasi 5 kwenye kamati ya uongozi. Badala yake
tumepewa nafasi 1 tu a Prof. Lipumba ambayo ameikataa kwa sababu si nafasi
ya haki.
11. Tuko hapa kwenye Bunge Maalum kutafuta katiba ya wananchi wa Tanzania,
hatuko hapa kutafuta katiba ya chama chenye wabunge wengi kuliko vyama
vingine kama anavyosema Mwenyekiti wa Bunge Maalum Samwel Sitta. Ili tupate
katiba ya watanzania wote lazima chama chenye wabunge wengi kitambue wingi
wao, na kiutumie wingi huo kuunganisha makundi muhimu yenye idadi ndogo ili
kutafuta katiba yenye maridhiano na inayokubalika na makundi madogo na
makubwa ndani na nje ya Bunge Maalum.
12. Michakato mingi ya kutafuta katiba mpya inaonesha kuwa vyama vilivyoko
madarakani huwa ni chanzo kikubwa cha kuvuruga mchakato wa katiba. Na sbb
kubwa ya kuvuruga mchakato husika huwa ni chama dola kutaka kuhodhi na
kulinda maslahi yake dhidi ya maslahi ya wananchi. Pamoja na uzoefu huu,
bado CCM hawataki kujifunza, wanataka kushinda bila kujali wananchi
watapata nini.
ANGALIZO;
Masuala hayo 12 yanaonesha wazi kuwa CCM hawana kabisa nia ya kuona nchi
inapata katiba inayokidhi matakwa ya wananchi. CCM wanataka kuchukua kila
kitu, wanataka kupata kila kitu, wanataka kuhodhi kila kitu, hawajali
wananchi wamesema nini.
Wasidhanie kuwa tulioko hapa Dodoma ni watoto wadogo, tutachukua hatua,
hatua stahili kwa wakati muafaka. Idadi yao na wingi wao havina maana
katika na juu ya maslahi ya taifa na matakwa na maoni ya wananchi.
MWISHO;
CCM watambue kuwa TUTAKULA nao sahani moja, hatutatumiwa kuwa mhuri wa
Maslahi ya chama chao na kwamba katiba mpya siyo hisani yao, ni matakwa
halisi ya watanzania na serikali na chama kinachoongoza dola lazima kitii
maoni ya wananchi na matakwa ya misingi ya kdemokrasia, na kwa sababu
mchakato huu umeshaanza lazima ufike mwisho. "Jini likitoka kwenye chupa,
halirudi"(hadithi za Alfu Lela Ulela).
--
*Yona Fares Maro*
Institut d'études de sécurité - SA
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/f5oe2cc8tvapcxunygv7dxvb.1395754007702%40email.android.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments