JINAI HAIZEEKI AU JINAI HAIOZI
"kwanza nipenda kuwaambia kuwa jinai haizeeki hata hao waliowaumiza akina DK.Ulimboka na Kibanda tutawakamata tu kwani bado uchunguzi unaoendelea………lakini mnapaswa kujifunza kuwa siku nyingine tukio likitokea mtuache tufanye kazi bila presha………hawa watuhumiwa wa Dk.Mvungi tumewakaamata kwa haraka baada ya kubaini kuwa tukio hilo halikuwa na chembe ya siasa…lakini yale matukio yaliyotanguliwa tulishindwa baada ya kuandamwa na mashinikizo hapa tunataka kuchunguza mara tunaambiwa na sisi ni watuhumiwa sasa tutajichunguzaje ndio maana tumechelewa kuwakamata watuhumiwa wale"Suleman Kova akiwajibu wandishi wa habaari leo,kwanini wamefanikiwa kuwakamataa haraka watuhumiwa waliomjeruhi Dk.Mvungi kabla ya wale wa Dk.Ulimboka na Kibanda
0 Comments