KUTOKUBALIKA KWA MUUNGANO WENYE MIUNDO WA SERIKALI MBILI NA TATU
Kwanza ifahamike kwamba zilizoungana ni nchi mbili tofauti, Tanganyika na Zanzibar na hivyo kabla ya muungano zilikuwa na heshma na hadhi sawa kama mataifa huru na bila shaka ndani ya muungnao inapaswa kuwa hivyo.
Kwa mtazamo huo basi ndani ya muungano wa serikali 2 na hata shirikisho la serikali tatu zilizopendekezwa katika rasimu utaratibu wa upatikanaji wa Rais wa muungano hauna budi kuwa ni kwa msingi wa kupokezana zamu ili kujenga sura ya usama na heshima kwa nchi mbili zilizoungana katika suala la uongozi wa juu wa nchi.
Wapo baadhi ya viongozi kutoka Bara wanabeza utaratibu wa urais kwa kupokezana zamu kwa kuweka hoja kwamba eti tusilazimishe utaratibu huo kwani itapelekea kupata Rais asie makini na mwenye sifa kutoka uopande wenye zamu kwa kumzuia mwenye sifa kutoka upande wa pili usio na zamu. Hoja hii si ya msingi na pia ni hoja ya uongo.
1. Ni hoja ya isiyo ya msingi kwa sababu hakuna taifa kati ya mataifa haya mawili ya Tanganyika na Zanzibar yenye historia ndefu kutokea uhuru. Hakuna nchi hata moja kati ya mbili hizi yenye ukosefu wa wasomi na wanasiasa wenye uzoefu na maarifa ya kutosha kuwa viongozi wakuu wa nchi wenye sifa. Mimi nadhani watoaji wa hoja hiyo wanakusudia kwamba inaweza ikafika zamu ya Zanzibar lakini Zanzibar huko kusiwe na Mgombea wa Urais mwenye sifa lakini upande wa Tanganyika ambao haupo katika zamu yupo mwenye sifa ila amekwazwa na kigezo cha zamu. Hii ni kwa kuwa siku zote watanganyika wasioipenda muungano wa haki na usawa wamekuwa wakiwazingatia wazanzibari kama ni watu wasijuwa kitu au wasaidizi tu katika utaratibu wa uongozi katika masuala ya Muungano pamoja na serikali yenyewe ya muungano.
2. Pia nii hoya ya kujifichia kwani utaratibu wa mwanzo wa muungano uliosema makamo wa Rais atakuwa Rais wa Zanzibar unafichua unafiki wa hoja hii. Ilipofika kipindi cha awamu ya pili, Rais wa Muungano alipokuwa Mzee Ali Hassan (anaedaiwa kuwa ni mzanzibari), Rais wa Zanzibar Mzee Idris Abdulwakil alikuwa Makamo wa Rais wa muungao pia mzanzibari. Msingi wa malalamiko ya upande wa bara hapa ilikuwa eti Zanzibar imetoa Rais wa muungano pamoja na Makamo wake. Hilo liliendelea kuwa halipendwi upande wa Bara mpaka pale katiba ilipobadilishwa mwaka 1994 ili isije ikatokea tena kama kipindi cha Mwinyi Zanzibar kutoa Rais na Makamo wake na badala yake kuwekwa mgombea mwenza ndio awe Makamo wa Rais.
Ili kuwaziba macho wana CCM wa Zanzibar walikubali hilo upande wa bara ulitumia kisingizio kwamba ni kumzuia Maalim Seif asiwe Makamo wa Rais wa Muungano pale atakaposhinda Urais wa Zanzibar kwani utalifanya baraza la mawaziri kuwa na mpinzani na hata Rais wa Muungano kuwa mpinzani pale Rais atakapopata dharura ya kuondoka katika kiti chake. Upande wa bara walipata kichaka hicho na wauza nchi wa Zanzibar wakaridhia kubadilishwa kwa utaratibu wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamo wa Rais. Hoja hapa ni kwamba hata watanganyika wenyewe hawapendi kuona Zanzibar inatoa viongozi wengi kwa wakati mmoja au kwa mfululizo wa vipindi, hivi inakuaje leo walete hoja ya kutokuwepo ulazima wa kubadilishana Urais kwa kuchelea Rais asiye na sifa?
Tukirejea katika mchakato wa maoni hata CCM wauza nchi waliopo Zanzibar wanasisitiza Urais wa muungano uwe ni kwa utaratibu wa zamu baina ya Tanganyika na Zanzibar, hivi ndivyo maoni yao yalivyokuwa na kwa hili tunawaunga mkono, wako juu ya mstari.
Sasa tuje katika msingi wa hoja hii, pamoja na kwamba upo ulazima wa kubadilishana Urais wa muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, suala hilo linajidhihirisha kuwa ni gumu na lisilowezekana kwa kutumia mfumo wa muungano wa kijamhuri uwe wa serikali 2 zilizopo au shirikisho la serikali 3 zilizopendekezwa na Jaji Warioba.
Kwa utaratibu wa chaguzi, ili kumpata Rais ambae atatoka upande mmoja wenye zamu ni lazima upande wa pili usiweke mgombea, na hili liwe ni kwa vyama vyote. Hii ni kwa sababu mgombea akisimama kutoka pande zote mbili uwezekano sawa wa kila mgombea kutoka pande mbili za muungano kuwa Rais upo . Kwa mujibu wa tofauti za kimitazamo za vyama vingi vya siasa za Tanzania vlivyopo si jambo la rahisi baadhi ya vyama kukubali utaratibu chama chao Fulani kisisimamishe mgombea wa Urais.
Hata hivyo tuseme hilo la upande mmoja kutoweka mgombea limekubaliwa na vyma vyote, basi sasa kutakuwa na kikwazo cha uhalai wa Rais huyo kwani upande ambao hauna zamu utalazimika kutokumpigia kura mgombea, kwa msingi kwamba zamu ya Urais ni kutoka upande mmoja na hivyo anapaswa kupata ridhaa ya nupande huo wenye zamu tu, upande wa pili haupaswi kuwa na ridhaa ya mgombea huyo ili kutoingilia matashi ya upande wenye zamu juu ya ni nani wanamtaka awe Rais wao. Hakadhalika Suala la upande usio na zamu kulazimika kutokupiga kura ya kumchagua Rais ambae ndie Mkuu wa nchi yao kunaondosha uhalali wa Rais huyo kwani bila shaka atakuwa hana ridhaa ya wananchi kutoka katika nchi ya pili inayounda muungano.
Hivyo basi utaratibu wa kupokezana Urais pamoja na ukweli kwamba hauepukiki baina ya pande mbili za muungano, utaratibu huo kwa kutumia mfumo wa serikali mbili zilizopo au shirikisho la serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Warioba hautekelezeki kwa kuzingatia utaratibu wa kiuchaguzi na misingi ya demokrasia.
Hivy basi mfumo pekee ni kutokua na serikali ya Muungano badala yake kuwe na chombo tu kinachounganisha nchi mbili kwa mfano tume ya Muungano au kamisheni ya muungano. Huu ndo muungano wa MKATABA. Nchi mbili zinabaki zikiwa na mamlaka yake na marais wake bila ya kuingiliana na mwenzake huku masuala machache ya muungano yakitaribiwa na chombo hicho.
"MBILI", "TATU" NO!, MUUNGANO WA "MKATABA" HAUEPUKIKI
JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA!!
-- Kwanza ifahamike kwamba zilizoungana ni nchi mbili tofauti, Tanganyika na Zanzibar na hivyo kabla ya muungano zilikuwa na heshma na hadhi sawa kama mataifa huru na bila shaka ndani ya muungnao inapaswa kuwa hivyo.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
0 Comments