[wanabidii] Mwaliko kwenye Kongamano la Amani na Usalama wa Taifa letu

Thursday, July 25, 2013
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM
Academic Staff Assembly
 

                                                                                                           24/7/2013

 Mwaliko kwenye Kongamano la UDASA Kuhusu Amani na Usalama wa Taifa Letu  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 28/7/2013
 
Kwa niaba ya Uongozi wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, napenda kukukaribisha kwenye kongamano  la kujadili Amani, Ulinzi na Usalama wa Taifa litakalofanyika tarehe 28/7/2013  ndani ya ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana hadi saa 12 jioni. Kongamano hilo litarushwa moja kwa moja na ITV.
 
Mada kuu ya kongamano hilo ni, "Mustakabali wa Amani na Usalama wa Wananchi na Taifa  Letu kwa Miaka 50 ijayo". Katika Mada hii kutakuwa na vipengele vikuu vitatu vitakavyojadiliwa:
a)     Mchango wa Vyombo vya Dola katika Amani na Utulivu wa taifa letu;
b)    Mchango wa Siasa na Dini katika kuimarisha Amani na Usalama wa Taifa letu;
c)     Mchango wa Vyombo vya Habari  katika kuimarisha au kubomoa Amani na Usalama wa taifa letu.
                                                    
Tutanguliza shukrani zetu za dhati kwa ushiriki  wako kwenye kongamano hili.
 
 
 
Asante
 
Faraja Kristomus
(Katibu – UDASA)
 


Mr. Faraja Kristomus
Department of Foreign Languages and Linguistics
University of Dar es Salaam
P.O.Box 35040, Dar es Salaam
Tanzania
Mobile: +255 787 52 53 96 / +255 717 086 135

"All human beings are equal except our beliefs, tribes and thinking, which are always accidents and never the essences of our humanity. We acquire them after getting out of the wombs of our mothers".

Share this :

Related Posts

0 Comments