Kubenea azua Utata Bungeni: Ashindwa kuwasilisha Nakala za Vyeti Vyake kwa Katibu wa Bunge!
HAMY-D
Kama ilivyoada katika bunge letu la JMT kuwa, kila tukifungua Bunge katika awamu mpya, basi kuna utaratibu wa wabunge kupeleka taarifa zao kwa katibu wa Bunge, hasa zile taarifa zinazohusu elimu na uzoefu tulionao kwenye maeneo mbalimbali au kwa lugha ilizoeleka na watu wengi tunaita CV.
Katika hatua hii ya kuwasilisha taarifa hizi muhimu, wabunge wote wamefanikisha uwasilishaji huu wa taarifa kwa ofisi ya katibu wa bunge kama ambavyo imepangwa, lakini ni mbunge mmoja tu hadi hii leo hajawasilisha taarifa zake kwenye ofisi ya Katibu wa Bunge, nae sio mwingine ni Saed Kubenea!
Taarifa hii ya kuwasilisha CV za wabunge ilitolewa tangu siku ya uzinduzi wa bunge uliofanywa na rais Dkt Magufuli na ilitakiwa kabla ya siku ya Desemba 4 taarifa zote za wabunge ziwe zimewasilishwa kwenye ofisi ya katibu wa bunge ili aweze kuziingiza kwenye tovuti ya bunge, lakini hadi leo hii ndugu yetu Kubenea bado tu hajawasilisha nakala za vyeti vyake kama ambavyo imeelekezwa na katibu huyo wa bunge.
Note: Hii taarifa imesambazwa kwa wabunge wa bunge la JMT ikimuhusu mbunge mwenzao na kwa sasa mjadala mkali sana unaendelea baina ya wabunge kuhusu suala hili la Kubenea kushindwa kuwasilisha nakala za vyeti vyake kwenye ofisi ya katibu wa bunge.
Kwa hisani ya Jf

0 Comments