[wanabidii] MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA VINASABA VYA BINADAMU, TANZANIA

Monday, July 22, 2013
WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI

MATUMIZI YA TEKNOLOJIA YA VINASABA VYA BINADAMU, TANZANIA

JULY, 2013

1.0  UTANGULIZI

Tekinolojia ya vinasaba vya binadamu inafanya kazi kwa kusimamiwa na sheria namba 8, sura ya 73, ya mwaka 2009. Sheria hiyo inaitwa The Human DNA Regulation Act, [Cap 73, 2009] ambayo inasimamia na kudhibiti matumizi ya tekinolojia ya vinasaba vya binadamu.

Mkemia Mkuu wa Serikali ndiye msimamizi wa utekelezaji wa sheria hii.

Taarifa fupi ya umuhimu wa tekinolojia ya vinasaba vya binadamu inavyosaidia katika matukio mbalimbali nchini Tanzania.

2.0 UCHUNGUZI WA VINASABA
Uchunguzi unaohusisha tekinolojia ya vinasaba, unahusisha vielelezo vinavyotokana au kupatikana katika mashauri au matukio yafuatayo:

a.    Mauaji
b.    Majanga
c.    Ubakaji
d.    Wizi /Wizi wa kutumia silaha.
e.    Uhamiaji
f.     Uhalali wa mzazi kwa mtoto
g.    Utambuzi wa binadamu
h.    Utambuzi wa Jinsi Tawala

3.0 MIFANO HALISI YA MATUMIZI YA TEKINOLOJIA YA VINASABA VYA BINADAMU
Baadhi  ya matukio au mashauri yaliyohusisha matumizi ya Tekinolojia ya vinasaba vya binadamu yamechanganuliwa  kama ifuatavyo:

s/n
Aina ya tukio
TUKIO
Matumizi ya Tekinolojia ya vinasaba vya binadmu
Maoni/hoja
3.1
Mauaji ya Albino na Vikongwe
·      SHINYANGA-3(2009)
·      KAGERA-3(2009)
·      SUMBAWANGA-2(2013)
Kesi  mbili(2)  tayari zilishatolewa hukumu kutegemea na matokeo ya uchunguzi wa DNA






3.2
Majanga
·      Milipuko-Mbagala(2010) DAR


·      Moto: Shule ya Idodi-IRINGA

·      Kuanguka kwa Jengo- Mtaa wa Kisutu.(2013).

·      Ajali ya Ndege Comoro.(2010)-Mafia/Dar
Askari 6 walitambuliwa na mabaki ya marehemu kuchukuliwa  na ndugu wa Marehemu kwa ajili ya kuzikwa.

Mabaki ya Marehemu, wanafunzi  12 walitambuliwa na makaburi kutambuliwa.

Mabaki ya sehemu ya miili ya marehemu 23 yaliweza kutambuliwa

Mabaki ya miili ya marehemu 25 iliweza kutambuliwa na ndugu kuchukua kwa ajili ya kuzika






3.3
Ubakaji/Mimba za utotoni.

Mkoa  wa MBEYA –(2013)


Uchunguzi umesaidia upelelezi na Mahakama
Katika kesi za kuwapa mimba mwanafunzi wa shule/wasichana chini ya umri 18.

3.4
Uhamiaji
·      Mbeya
·      Ngara-Kagera: Mwanachi kutoka nchi nya nje kudai kuwa na uhusiano na na ndugu ntanzania


Tekinolojia ya vinasaba ilitumika na kudhihirisha kuwa hawana uhusiano na wananchi waliowataja nchini Tanzania






3.5
Wizi/wizi wa kutumia silaha
·      Wizi wa benki NMB(2006)

·      Wizi wa benki ya West Bureau De Change

Uchunguzi umesaidia upelelezi na Mahakama katika kubaini wa husika









3.6
Human trafficking (biashara haramu ya binadamu)
·      Miili ya binadamu iliyopatikana: Morogoro
·      Dodoma
·      Kibaha
Utambuzi wa binadamu kwa miili iliyopatokana






3.7
Uhalali wa mzazi kwa mtoto
Katika kipindi cha Mwaka 2010-2012:

51.68%-Kuhusisha(watoto ni wao)
48.32%-Kutohusisha(watoto sio wao)








3.8
Utambuzi wa Jinsi tawala
Katika kipindi cha Mwaka 2010-2012
2.49%-Utambuzi wa jinsi tawala


4.0 MATARAJIO YA BAADAE

Mkemia Mkuu wa Serikali  kupitia wizara mama ya Afya na Ustawi wa Jamii inamatarajio yafuatayo:
          i.        Kuhusisha Nyanja za tafiti
          ii.        Kuwepo kwa database ya vinasaba vya binadamu
          iii.        Usajili na ukaguzi wa taasisi zinahusisha matumizi ya tekinolojia ya vinasaba vya binadamu

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/groups/opt_out.
 
 

Share this :

Related Posts

0 Comments