Madai ya kingunge kwamba CCM ili violate kanuni kumpitisha mgombea urais yamekua ya mda mrefu sasa na amekua akiyarudia mara kwa mara. CCM tuliona kikifanya mikutano yake mbali mbali kuhakikisha kinapata mgombea bora mwenye sifa na aliechunguzwa atasimamia maslahi ya taifa. Taarifa zinasema Lowassa alikatwa kwa sababu ya "fail lake kujaa uchafu".Kila nchi lazima iwachunguze wagombea wake na kama taarifa hizo zinavyosemekana Lowassa alikosa vigezo na si kila taarifa itawekwa wazi for public consumption.
Mi naamini Lowassa Kama wagombea wengine wengi waliojitokeza kupitishwa na chama cha mapinduzi walikua na haki sawa na hakukatwa mwenyewe, hata makamu wa rais alikatwa, waziri mkuu alikatwa, kwanini Lowassa aonekane ana haki kuliko wagombea wengine? Kwanini lazima awe yeye?
CCM ilimpata mgombea wake kupitia vikao mbalimbali kuanzia kikao cha kamati ya wazee, maadili mpaka mkutano mkuu. Tujiulize CHADEMA walifanya kikao gani kumptisha Lowassa? Inamaana u dictator uliofanywa na mbowe ni SAWA? Lowassa alipitishwa na vikao gani? Hichi ndio chama makini kinachotaka tukikabidhi nchi>? KAMA TUNAONGELEA KUVUNJWA KANUNI BASI KANUNI ZILIVUNJWA NA UDIKTETA WA HALI YA JUU ULIONYESHWA KUMPITISHA LOWASSA KUA MGOMBEA CHADEMA.
Lowassa angetakiwa ahimize demokrasia ifanyike Chadema ili aonyeshe jinsi alivyochukizwa na yaliyotokea ndani ya mchakato wa kumpata mgombea ndani ya chama cha mapinduzi. CCM walivunja kanuni kwasababu tu jina la Lowassa Halikurudi, Je nani hata alipata fursa ya kuchukua form CHADEMA?TAFAKARI.
Uncategories
[wanabidii] Swali kwa Kikunge: Labda kanuni hazikufuatwa CCM kumpitisha Lowassa: CHADEMA walifuata
Related Posts
- [wanabidii] New content updates
- [wanabidii] New content updates
- [Mabadiliko] Katika Nyakati Hizi Msiwasahau Watu Wa Aina Ya Gerson Hosea Malangalila Lwenge ...!
- [wanabidii] Tumeboresha huduma
- [wanabidii] Guidelines on Patentability and Access to Medicines
- [wanabidii] FAHAMU JINSI #RECRUITME INAVYOWEZA KUKUPA UJUZI UTAKAOKUSAIDIA KUPATA KAZI UITAKAYO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Comments