[wanabidii] Lowassa na UKAWA wamesahau kuwa SIASA NI SAYANSI

Sunday, October 04, 2015
Quote Originally Posted by Nambalapala View Post
Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi watanzania wenye sifa za kupiga kura na waliojiandikisha ni milioni 23.7 katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25. Huku vyama vilivyosimamisha wagombea katika nafasi ya urais ni nane. Lakini mchuano upo baina ya Chama Tawala CCM na chama kikuu cha upinzani nchini Chadema. CCM inawakilishwa na Dkt. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI ilihali Chadema inawakilishwa na Edward Ngoyai Lowassa wakipewa upambe toka vyama vya CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD.

Wataalamu wa sayansi ya siasa,wachambuzi na wanasiasa nguli wameandika sana juu ya mambo mbalimbali yanayoweza kukipa chama au mgombea ushindi kwenye kinyang'anyiro chochote cha urais mahali popote. Kutokana na Machapisho yao yaliyotokana na tafiti pamoja na uzoefu wao katika ulingo wa siasa wanasema yapo mambo manne yanayochangia ushindi; Utambulisho na Nguvu ya chama, Kuwepo madarakani, Ufahamu wa wapiga kura na historia ya wapiga kura.

Naomba kuanza na Utambulisho na Nguvu ya chama........
Kwa mujibu wa "Club effect" ni kuwa katika uchaguzi wa rais 90% ya wanachama huwa wanakipigia kuwa chama chao na 10% husaliti. Kwa mujibu wa maelezo haya 90% ya wanachama 8,400,000 wa CCM ni 7,600,000. Sasa ili kushinda uchaguzi kwenye nchi yetu mwaka huu 2015 lazima mgombea apate zaidi ya kura milioni 12;hivyo CCM watahitaji kura milioni 5 tu kutangazwa washindi. Namna chama kinajitambulisha kwa wapiga kura kwa kumtambulisha mgombea wake kunachangia 5% ya wapiga kura wote ni 1,185,000.

Eneo la pili kuwepo madarakani kwa chama au mgombea husika "Incumbent performance" ambapo kunachangia 15-30% wapiga kura wote. Wataalamu wanasema kama serikali ya chama husika haikufanya vyema basi watapata chini ya 30% ya wapiga kura wote na kama watakuwa walifanya vizuri watapata 30% ya wapiga kura wote. Ni ukweli kuwa CCM yapo maeneo waliyofanya vizuri na yapo ambayo hawakufanya vizuri na mgombea vivyo hivyo kwa maana nyingine 15% ya wapiga kura ni 3,555,000.

Pia wanasema uelewa/ufahamu wa wapiga kura unachangia 5% ya wapiga kura wote "Dunning krugger effect". Yaani watakaochagua baada ya kuwasikiliza na kuchambua sera na kisha kutoa kura yake kwa kujiridhisha mgombea husika amemridhisha. Maana yake ni kura 1,185,000.

Ndiyo maana kwa hesabu hizo CCM wanajipa uhakika halafu wengine wanasema CCM wanakiuka demokrasia kumbe wamesahau siasa ni sayansi. Mpaka sasa CCM katika kila Mkoa,kila wilaya,kila jimbo na baadhi ya kata katika jimbo husika mgombea wao wa urais amefanya mikutano ya kampeni ambayo inakadiriwa mpaka sasa amefanya mikutano zaidi ya 115 na isiyo rasmi ya kusimamishwa kwenye vijiji na barabarani 436. Ambapo mikutano 49 imerushwa LIVE na Star TV hivyo kuwafikia watanzania karibu wote.

CCM ikiwa imefanikiwa pia kuungwa mkono na wasanii wote maarufu kwenye maigizo na muziki hivyo kuteka kura nyingi sana za rika zote vijana,wanawake na wazee. Kete nyingine ni utamaduni wake wa kampeni za ustaarabu zisizo na fujo wala vurugu ambazo zimewavutia wengi kama inavyooneka hapa. Hivyo CCM kushinda kwa zaidi ya 62% ukikataa utakuwa unaendeshwa kwa hisia na mihemko na si uhalisia.Utamaduni wa CCM kuamini ahadi ni deni kwa kutekeleza ahadi walizozitoa kwa watanzania kupitia ilani zao na ahadi binafsi za wagombea urais ndio siri ya kuaminiwa zaidi.....Jioneee!!!!!!!!!!

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments