Tanzania iko kwenye mchakato wa kumpata rais wa awamu ya Tano. wagombea watatu Yaani Anna Mungwira wa ACT Wazalendo; Edward Lowassa wa CHADEMA/UKAWA na Dr John Magufuli wa CCM wanachuana kwa namna ambayo mmoja wao anaweza kushinda uchaguzi huu. Huenda ikaja kama kichekesho kumuingiza Anna lakini tufuatilie mambo kadri tunavyosogea karibu na uchaguzi tutaona.
katika uchaguzi huu karibu watanzania wote wanataka mabadiliko. Wako wanaoona kuwa mabadiliko yatapatikana kutoka CCM na kuna wasioamini kuwa CCM inaweza kuleta mabadiliko. Kuna wanaosema mabadiliko nje ya CCM labda yawe yanatoka ACT Wazalendo na sababu yao ni kuwa wasimamizi wa mabadiliko ndani ya UKAWA ni wanaCCM ambao wamekimbia baada ya kukosa nafasi wala si kutokana na ubovu wa CCM
Siku chache zilizopita Mzee Kingunge amejitoa CCM. sipendi kujadili sababu za kujiondoa lakini sasa anajitokeza kwenye jukwaa la CHADEMA akitaka kufanya kazi moja tu Kuonyesha ubovu wa serikali ya Kikwete.
Sishangai. Sishangai maana nilishangaa siku zile alipoamua kumuunga mkono mmoja wa wagombea na baada ya kushangaa nilimsoma na kumuelewa Kingunge.
Ninachokiona na kukishangaa ni hiki: Kingunge anataka kuwasaidia watanzania kufanya maamuzi siku ya tarehe 25 October kwa kumjadili kiongozi anayemaliza muda wake. Hivi kingunge anapoanza kumjadili Kikwete inatusaidiaje kumpima magufuli au Lowasa ambao wamekuwa viongozi katika serikali za CCM? Angekuwa jukwaa la Anna wa ACT ningemuelewa.
Kingine ninachokishangaa ni kusimama jukwaani kumkosoa rais anayemaliza madaraka yake wakati Kingunge alikuwemo ndani ya mfumo na kutoka kwake si kwa sababu ameukosoa ikashidikana bali mgombea wake hakupata nafasi ya kugombea.
lakini jambo jingine anawasaidia nini watanzania kumkosoa Kikwete ambaye amekosolewa tayari na wagombea wote ikiwa ni pamnoja na Mgombea wa CCM? hajamsikia Magufuli akikosoa uzembe uliopelekea maadili kuporomoka? hajamsikia magufuli akisema mafisadi wote walioko CCM na waliokimbia wanasubiriwa mahakama maalum itakayoundwa baada ya uchaguzi?
Nadhani si kosa kufikiri na kusema kuwa Kingunge anaota. SAWASAWA????
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments