1) Katiba mpya. haiepukiki swala la katiba mpya lazima lijitokeze. CCM ikijaribu kulifumbia macho UKAWA italileta na lazima litaitesa tu. Wananchi tunataka katiba na hakuna mwenye kiganja cha kuzuia mafuriko ya agenda hii.
CCM inaweza kuamua kushupalia katiba ya Sitta na Chenge. Ikijaribu iwe tayari kupoteza. Lakini ninajua kuwa hata wakati inapitishwa na wabunge wa CCM walijua wanavunga. Walitegemea popularity ya chama na wingi wa wabunge katika bunge la katiba. Sasa naamini nao wanajua katiba ya wananchi ni lile toleo la Pili la tume ya Warioba.
Je Wako tayari kuyameza matapishi na kutelekeza katiba ya Chenge? Aibu itawapata au siasa ndivyo ilivyo? watasemaje kuhusu fedha zilizotumika ambazo wangesikiliza upinzani zingepona? Au watamtwika mziko JK na kuwa wapya katika hilo? Je ikitokea wakayameza matapishi yao na wakaibuka na mpango wa kuileta katiba inayotakiwa na wananchi UKAWA itabaki? Kufanya nini na agenda yake itakuwa ni nini?
La pili ambalo iweje iweje lazima lijadiliwe ni swala la Rushwa na ufisadi. Haiwezekani tanzania ikaendelea hata wapangani wa mipango makini kama Lipumba wangekuja na mipango gani Rushwa na ufisadi haviwezi kuruhusu tanzania ikaendelea. Mambo mengi yamekwama kwa sababu hiyo. Kuna wakati sheria zimetungwa ili kushibisha watu. Tunakumbuka swala la mikanda ya magari, Speed governers taja na mengine. Ilikuwa rushwa na ufisadi. CHADEMA ilijipambanua kwa kuileta agenda hii na kwa kweli CCM imeteswa na Chadema kwa sababu hiyo. Tanzania haiwezi kuendelea bila kuyashughulikia matatizo hayo kwanza. Mabadiliko yanayohubiriwa ni kuanza kubadili hapo ndipo tanzania ifaidi raslimali zake.
Baada ya Mheshimiwa Lowasa kujiunga na Chadema haiwezekani kabisa Chadema ikatumia maneno iliyokuwa ikiyatumia kuongelea ufisadi. Ikifanya hivyo itakorofishana namfadhili wake Lowasa. Huwezi kuongelea ufisadi bila kutaja mafisadi kama usivyoweza kuongelea wizi bila wezi. CHADEMA itakuwa tayari kushupalia kauli yake juu ya mafisadi mgombea wake wa urais apone, au itaitelekeza lugha yake na kula matapishi yake? Ikifanya hivyo itapona au ndiyo itakuwa inajizika mchana kweupe? CCM inatarajia kunufaika vipi katika hili? inaweza kunyamaza na kuendelea na mafisadi wake waliobaki ndani yake maana hakuna mashambulizi tena. Lakini inaweza kuendelea kujivua magamba kama ilivyoonyesha katika mchakato wa kumtafuta na kumpata mgombea urais na hivyo kuteka sera za mpinzani wake Chadema. Hii nayo ipo. Watanzania kwa sasa wanaanza kwenda na hoja badala ya rangi za vyama.
Yaani kutumia nguvu ya hoja badala ya hoja ya nguvu.
Naona kama haya ni mambo muhimu ya kujiandaa nayo huko tuendako
Elisa Muhingo
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya
kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility
for any legal consequences of his or her postings, and hence
statements and facts must be presented responsibly. Your
continued membership signifies that you agree to this
disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the
Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails
from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments