[wanabidii] BIRTHDAY PARTY BENDI YA FM ACADEMIA AGOSTI 21

Saturday, August 08, 2015
BIRTHDAY PARTY BENDI YA FM ACADEMIA AGOSTI 21

Na Happiness Katabazi
BENDI ya FM Academia "Wazee wa Ngwasuma" , Agosti 21 Mwaka huu, itafanya sherehe ya kukata na Shoka ya kukumbuka kuanzishwa kwake miaka 18 iliyopita.

Akizungumza na Mwandishi wa Habari hizi, Mhasibu wa Bendi hiyo, Calvin Mkinga alisema sherehe hiyo ambayo imepewa jina la Birthday Party FM Academia Band ,itafanyika tarehe hiyo saa moja usiku Katika ukumbi wa Arcad House Mikocheni Dar Es Salaam, na kwamba Maandalizi yote yameishakamilika.

Mkinga alisema kiingilio ni Sh. 10,000 na kwamba siku hiyo ambayo itakuwa ni siku ya Ijumaa, wimbo mpya wa Dada wewe uliotungwa na mwanamuziki King Blaise ambao utaanza kupigwa kwenye redio mbalimbali leo utatambulishwa rasmi siku hiyo pamoja na nyimbo nyingine na akawaomba mashabiki na wapenzi wa Bendi hiyo kujitokeza kwa Wingi ili waje kusherehekea pamoja sherehe hiyo ya kihistoria.

"FM Academia inajisikia faraja sana kuona BendI hiyo inatimiza Miaka 18 kwasababu ni umri mkubwa na kuna baadhi ya bendi zilitamani zitimize umri hiyo zilishindwa na kufa mapema kwasababu ya kushindwa kuimiri Changamoto mbalimbali.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Blog: www.katabazihappy.blogspot.com
8/8/2015.


Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments