Napenda kuchukua fursa hii adhimu kumpongeza kwa dhati kabisa Rais mstaafu, Mh William Benjamin Mkapa, kwa kuwaambia watanzania ukweli pasipo kumumunya maneno, kupepesa macho wala kutikisa masikio. Ijapokuwa hata makada wengine wa CCM wamekuwa wakisema ukweli katika kauli zao mbalimbali lakini Mh Profesa Mkapa amesema ukweli zaidi. Ametamka ukweli usioweza kupingwa na mtu yeyote, awe zezeta au mwenye akili zilizotimia. Nianze na kauli za mkapa kabla sijaangazia kauli za makada wengine waandamizi wa CCM.
Watanzania ni MALOFA na WAPUMBAVU. Hapa naomba nisisitize kauli hii ya Profesa Mkapa. Sio tu kwamba watanzania ni malofa mifukoni mwao lakini pia ni malofa katika vichwa vyao. Omba sana uwe lofa mifukoni lakini sio kichwani. Ukiwa lofa kichwani akili zako zitafanana na za kuku au konokono. Ulofa wa watanzania ndio unaowapelekea kuwa WAPUMBAVU. Ni bahati mbaya kwamba watanzania wengi ni malofa na pia ni wapumbavu. Ulofa huzaa upumbavu na upumbavu huzaa ulofa. Ulofa na upumbavu ni sawa na kuku na yai. Haiwezekani kutenganisha sifa hizi mbili kama ilivyo vigumu kutenganisha kuku na mayai.

Ni ulofa na upumbavu ndio unaopelekea watanzania kusomesha watoto wao kwenye shule za kata—shule ambazo hazina walimu, madawati, vitabu wala maabara huku wadosi wakisomesha watoto wao kwenye shule za intaneshno na englishi mediamu. Na sio tu kwamba ulofa na upumbavu wao huwafanya wasomeshe watoto wao kwenye shule hizo bali pia huwafanya washindwe kuwanunulia watoto wao walau kigoda cha Tsh 500/= kwa ajili ya kukalia wawapo darasani. Kwa ujumla, ulofa ndio chanzo cha watanzania kutopata huduma muhimu za kijamii.

Aidha ulofa na upumbavu wa watanzania hupelekea kutibiwa kwenye hospitali za umma huku wadosi wakitibiwa India, Ujerumani, Uingereza na kwingineko huko ughaibuni. Hali kadhalika ulofa huwafanya wakose pesa za kununua dawa kwenye maduka yaliyopo ndani ya hospitali na pia kushindwa kuwanunulia wagonjwa wao magodoro na vitanda ili pindi waendapo hospitali walalie. Kama mtu unakosa Tsh 200/= za kununua panadol kwenye maduka yaliyomo ndani ya hospitali za umma utasemaje wewe sio lofa?

Ni ulofa huo huo ndio unaopelekea watanzania kuuza kura zao kwa bakuli moja la ubwabwa, kopo moja la mataputapu, gram 200 za chumvi ya Tsh 100/=, kofia na vitenge kutoka kwa wadosi wenye nazo. Pia ulofa wetu unatufanya tukose Tsh 50/= za kununulia fungu moja la mchicha kwenye soko la Mchambawima wakati wadosi wana uwezo wa kuchukua milioni 10 za kununulia mboga. Ulofa wa wazazi wetu ulisababishwa tusomeshwe kwenye shule za kata na hivyo kukosa fursa ya kupata elimu iliyo makinika na itakayotuwezesha kutoa "ushauri" ili tulipwe Tsh 1.6 bilioni kwa kazi hiyo ya kutoa "ushauri wa kiufundi". Huu ndio ukweli ambao watanzania hamuwezi kuupinga. Kama kuna mtu atapinga basi anahitaji akapimwe akili zake Milembe.

Jamani hebu tuwe wakweli. Ulofa ni sifa ya watanzania na wala hakuna anayeweza kukataa ukweli huu. Tunapaswa kumpongeza Mh Mkapa kwa dhati kabisa kwa kauli zake za kweli na zinazozingatia maslahi mapana ya kitaifa.
Sasa nisemee ukweli uliomo kwenye kauli zingine zilizowahi kutolewa na makada maarufu hapa nchini. Oil ikishatumika sana kwenye gari huchafuka na hatimaye humwagwa chini. Naunga mkono kwamba watanzania ni OIL CHAFU. Kama mmetumiwa tangu mwaka 1961 mpaka leo na hamna namna nyingine ya kujinasua kutoka kwenye matumizi hayo mtakataaje kuitwa oil chafu? Nawashangaa sana! Ndio, sisi watanzania ni oil chafu…baada ya kutumiwa kwa muda mrefu sasa hatuna thamani tena…tunahitaji kumwagwa chini ili tusije tukaleta mushkeli kwenye gari la mabwana wakubwa.
Mtu akishatufuna muwa au kula ndizi hutupa MAKAPI chini na kuyaacha yaozee pale. Hakuna mtu mwenye akili zilizotimia ambaye akimaliza kutafuna muwa au ndizi huhifadhi makapi. Baada ya kutumikishwa kwa zaidi ya miaka 54 sasa watanzania tumekuwa makapi. Hatuna tahamani tena mbele ya watafunaji. Tunapaswa ama kuchomwa moto au kuzikwa ardhini tuwe mbolea. Sharti tukubaliane kwamba watanzania tumetafunwa na kunyonywa sana hadi tumebaki makapi tupu tusiokuwa na chembe ya thamani mbele ya watafunaji. Na uzuri ni kwamba mtu akishashiba hakumbuki kama kesho atapata njaa. Ifike wakati tukatae kutafunwa na kubaki makapi kama tulivyozoea kutafunwa kila msimu wa mavuno unapokaribia. Yatupasa tutengeneze sumu kali ambayo itawafanya watafunaji washindwe kututafuna tena msimu huu wa mavuno.
VIBAKA huiba mali za watu wengine baada ya kukosa kazi ya kufanya au baada ya kutelekezwa na jamii inayowazunguka. Baada ya serikali kuuza viwanda na ardhi kwa mabeberu na magabacholi, watanzania wamebaki hawana kazi wala ardhi ya kulima. Wamegeuka kuwa vibaka na kero kwa wawekezaji. Ndio maana kila kukicha tunashuhudia vibaka hawa wakipora mali za wawekezaji. Dawa yao ni kuwapiga mabomu na virungu mpaka watie akili. Hakuna hata haja ya kuwafikisha mahakamani—wananchi wenye hasira watashughulika nao mpaka wajute kuzaliwa kwenye ardhi hii ya Tanzania. Waacheni "wawekezaji" waifaune nchi na "wawekezwaji" wafurahie 10% zao walizozipata baada ya kuuza viwanda na kupora ardhi ya watanzania.

Kila mwenye akili timamu atakuwa ameng'amua ukweli uliojificha kwenye mafumbo haya yanayosemwa na makada kila kukicha. Watanzania mnapaswa kubungua bongo zenu muelewe kwamba mafumbo haya hayasemwi kwa bahati mbaya bali yanasemwa kwa makusudi ili kuwafungua akili zenu zilizofungwa na wachawi kutoka kuzimu. Lakini kwa kuwa mu malofa na wapumbavu, itawachukua muda mrefu kuelewa ukweli uliojificha kwenye mafumbo haya. Na akili zenu zikifunguka mtakuta rasilimali zote za taifa zimefyonzwa na kusalia makapi. Kwani hamuoni jinsi ardhi yetu inavyochimwa na kuachwa mahandaki? Ardhi isiyokuwa na kitu ni sawa na makapi. Ni juu yako ewe mtanzania kuamua uendelee kubaki kwenye fungu la malofa, wapumbavu, oil chafu, makapi na vibaka. Saa ya kujikomboa kutoka kwenye makundi hayo ni sasa. Fumbo mfumbie mjinga, mwerevu ataling'amua. Tafakari, chukua hatua!

0 Comments