[wanabidii] Kiteto tumejipanga na Magufuli wapinzani wataisoma mwaka huu

Tuesday, July 21, 2015
Na Mkulima wa Kiteto

Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mkoani manyara tumejipanga vilivyo wapinzani wajiandae kisaikolojia kuisoma namba, kuanzia hapa Kibaya, Matui, Ngusero, Dosidosi, Kongoli, Mbigili,Lang'otoni, Lairelo, Njoloo, Mbeli pamoja na Mrijo juu na chini na sehemu zingine.

Mwanzo tulikuwa na Mashaka na mchakato wa weagombea urais wa ccm kutoka na mgombea mmoja kuwapa kiburi watu wa jamii Fulani hapa kiteto na kusababisha mapigano ya mara kwa mara kati ya wafugaji na wakulima.

Lakini wana kiteto kwa ujumla tuna imani kubwa na dr. Magufuli kutokana na utendaji wake serikali hususani kwa kusimamia ujenzi wa madaraja yakiwemo ya hapa kiteto kama madaraja chemchem, Ngarenalo na mengineyo

Pia tunaamini Dr.magufuli atamaliza uhasama uliopo baina ya wafugaji na wakulima inayotokea hapa ambapo mwaka wa jana watu kadha walipoteza maisha kutoka pande zote mbili za wafugaji na wakulima haswa katika maeneo ya Matui, Chekanao, Lang'tomoni pamoja na Irela.

Tunapenda kumpongeza Dr. Magufuli na Rais Jakaya Kikwete sasa Kiteto tumeanza kuiona lami katika maeneo ya kibaya na na ujenzi wa barabara zingine za kiwango cha lami unaendelea, hilo tukio la kwanza kwa wakazi wa halmashauli ya wilaya ya Kiteto kuwa na lami tangu uhuru hatukuwahi kuwa na lami tulikuwa tukiiona kwenye tv na kuisikia kwa wenzetu.


--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments