Ndugu Zangu.
Ninajua wengi wetu mmechoka kufikiri na kujadili kwani mnaonekana kama mmekata tamaa vile? Sasa kama kweli mmekata tamaa hii nchi mnataka kuwaachia kina nani na ni yetu sote?:
Ninaomba nilete agenda mbili ambazo labda vyama vya siasa vinaweza kuangalia uwezekano wa kuziweka kwenye manifesto ya campaign kwa ajili ya uchaguzi ujao.
1. Hili la musirikali kuwa mfanyabiashara na mfanyabiashara kuwa musirikali bila kuwa na sheria, mbinu za kuwatenganisha, mkakati na wajibu wa kuhakikisha watu hawa wamefungiwa gavana ili wasije wakazidisha kwa kutumia nafasi zao kwa manufaa yao binafsi badala ya kwa manufaa ya nchi yetu tukufu. Hili mnalionaje? Jadili
2. Hili la mkulima mdogo na mfanya biashara mdogo "maachinga" kujengewa uwezo kwa kutumia mbinu za kibiashara kwa kuhakikisha gharama hizo zibebwe na gharama za bidhaa au zao linapofika zokoni bila kuathiri ushindani wa kushiriki kikamilifu kwenye uchumi huria. Hii inaweza kuwa mbinu sahihi za kukabiliana na umaskini uliokithiri hasa katika kuzalisha, kusindika na kuuza mali au bidhaa zilizoongezewa thamani. Kwa mfano mkulima wa mahindi auze unga wa mahindi? mkulima wa pamba auze pamba iliyochambuliwa ili aweze kupata zile mbegu za pamba na kuzisindika na kutengeneza mafuta, mashudu na mazao yeyote. Au mzalishaji wa mpunga aue soko la mpunga na auze mchele uliopangwa kwenye madaraja. Hii imekaaje? Itasaidia? Tujadili
3. Kwa machinga apewe mbinu za kuongezea thamani wa kile anachouza ili kuweza kujenga hoja ya kukiuza kwa bei kubwa zaidi kuliko bei za hibyo bidhaa kwenye duka la kawaida? Kwa mfano wamachinga kujenga umoja kwa kushirikiana kuongozea label ya bidhaa na kuuza bidhaa ile kutumia mbinu na mikakati tofauti kwa mfano kuuza kutumia simu za mkononi na kupeleka nyumbani kwa mnunuzi?
Mbinu hizi za kuongezea thamani zinaweza kutumia kwenye migodi yetu, gesi, petroli, bidhaa za asili, na huduma mbali mbali ambazo zitaboresha kipato chetu. Kwa mfano Tanzania tunapata asili mia 3 % ya thamani ya kilo ya kahawa inayouzwa pale London Supermarket. Inatufanya sisi kuwa wafadhili badala ya wao wasungu kuwa wafadhili. Jadili
Tuko pamoja
Herment A. Mrema

0 Comments