[wanabidii] Ombi maalumu kwa afande Kova

Saturday, March 14, 2015
Namuomba afande Kova atumie kasi ile ile aliyotumia kuwashtaki makada wa Chadema, kuhakikisha wote waliopanga njama za kumwua Dr Slaa wanafikishwa mahakamani!

Vile vile namuomba afande Kova ahakikishe anawafisha mahakamani wale waliomtesa Dr Ulimboka kwa kuwa walishatajwa kwa majina! 

Halafu namuomba afande Kova ahakikishe kwa kasi ile ile anawafikisha mahakamani wale waliomtesa kiongozi wa vijana waiopitia mafunzo ya Jeshi la kujenga taifa.

Mwisho namuomba afande Kova akumbuke kuwa duniani tunapita na kile tupandacho duniani ndicho tutakachovuna siku ya qiyaamah! 

Share this :

Related Posts

0 Comments