Att: Peter Kibatala;
-- Huyu jamaa analalamika hakupati!
My learned brother Kibatala, P.
Nimepata fursa ya kusoma response yako juu ya mambo kadhaa niliyoyabaini juu ya sakata la tamko la mmoja wa viongozi wa CHADEMA kuwa Mhe. Zitto Kabwe amefukuzwa uanachama wa CHADEMA baada ya Mahakama kuu kutupilia mbali maombi yake kutokana na pingamizi la awali lililotolewa na mawakili wa CHADEMA kukubaliwa kwa kuzingatia hoja mbili za pingamizi hilo kati ya tano zilizokuwepo.
Nianze kwa kukushukuru wakili kibatala (former Vice president wa TLS) kwa kunitaka nifanye marejeo ya kesi ulizozitaja nami nakuahakikishia kuwa nazifahamu na contents zake zote ila kurudia kuzirejea si vibaya. Nitafanya hivyo. Lengo langu si kuonesha umahiri wa kurumbana kisheria katika mtandao huu kwani kama nataka hayo tutakutana sehemu sahihi na siyo humu mtandaoni ilia nataka kukuhakikishia kuwa nakubaliana na hoja yako kuwa ni jukumu la mwenye kesi kujua kesi yake iko lini pamoja na wakili wake, lakini pia ni jukumu la mahakama kuwawezesha kujua kesi hiyo ipo lini maana bila hivyo basi summons zingekuwa hazitolewi na Mahakama kuwajuza parties kesi zao zimepangwa lini hasa kwa kesi kama hii ambayo wewe mwenyewe umekiri kuwa karani aliagizwa na jaji amfahamishe wakili wa Zitto kesi imepangwa lini. Kwa kufanya hivyo Jaji alijua wajibu wa mahakama ni upi na wajibu wa wakili ni upi. Hoja yako ya msingi hapa ambayo in mashiko ni kwamba kesi hiyo ilikuwa inakuja kwa ruling na pande zote zilishatoa hoja za maandishi. Awali tulipotoshwa ama na vyombo vya habari au wakili wa mlalamikaji/mpeleka maombi na Mpeleka maombi kwamba kesi hiyo ilipangwa kusikilizwa kwa tarehe tofauti na tarehe ilipotolewa ruling, ndiyo maana katika hoja yangu nilisema KAMA NI KWELI KAMA ILIVYORIPOTIWA NA VYOMBO VYA HABARI. Kwa kuwa umelitolea ufafanuzi hilo sioni sababu ya kuendelea kulumbana juu ya tarehe hiyo ya maamuzi na kutokuwepo kwa upande mmoja maana tayari kesi ilishasikilizwa interparties kwa njia ya maandishi.
Hoja yako kuwa KATIBA YA CHADEMA haiwezi kuwa void ab initio kwa kukataza wanachama wao kwenda mahakamani hilo mimi sikubaliani nalo na ningekuwa mwanachama wa hicho chama ningekwenda mahakamani kupinga ibara ya Katiba hiyo kwa kuwa ni unconstituitional. Kama unazuia watu wasiende mahakamani na hutendi haki kwa watu hao unataka waende kulalamika wapi? Waje kulalamika kwako mwenyewe huyo huyo ambaye hutendi haki kwao? Can a judge be a judge of his own case? Does it fall in the ambit of the principles of natural justice?Does CHADEMA adhere to the Rule of law principles when it comes to the reality that one wishes access justice through the temples of justice in this country? The answer is definitely NO kama hamuwezi kuruhusu wanachama wenu kuwapinga au kukipinga chama mahakamani kama mnaona kwa kufanya hivyo ni makosa. Kama aliye madarakani hapendi kukosolewa mahakamani ili mahakama itowe tafsri sahihi kwa kile kinachobishaniwa ni hatari sana kwa ustawi wa demokrasia ya nchi hii. Kama hutaki Chama kishitakiwe je siku mkichukuwa nchi mtakubali Serikali ishitakiwe? au ndo mtu/ raia wa nchi hii akiishitaki basi anakosa sifa na haki ya kuwa raia wa nchi hii kwa kuwa tu kaishitaki serikali kwa kuwa anaona haki yake imevunjwa, inavunjwa au inaelekea kuvunjwa? Kweli CHADEMA kinaweza kutoka wenye UMMA wa watu kifua mbele na kujinadi kuwa ni chama kinachofuata misingi ya kidemokrasia huku hakiamini kuwa mahakama ndicho chombo cha juu kabisa katika utoaji haki? Kwa hilo kaka yangu msomi mwenzangu kubali kuwa mmepotoka na wewe ninavyokufahamu kama makamu rais wangu uliyepita huamini katika hilo ila siasa zinakupofusha. Imefika muda wa kuchagua mbivu na mbichi. Achana na mbichi chagua mbivu. Acha giza, chagua nuru. Acha uongo chagua ukweli. Acha dhuruma ya haki za watu chagua haki. Usiwe kama baadhi ya wanasheria na mawakili waliopotea sifa za uanasheria wa kweli na kubaki kuropoka mambo ya kisiasa na kukanyaga taaluma zao. Uliona wapi wakili makini anaropoka tu kuwa fulani kuanzia leo si mwanachama wa chama fulani huku akijua kabisa kwanza yeye siyo proper authority ya kutamka hivyo lakini pia hata kama angekuwa ni proper authority anafanya hivyo bila kufuata utaratibu unaotakiwa. Hivi mahakama ikitoa judgment na execution ya decree inafanyika hapo hapo?hao ndo wanasheria walio CHADEMA wanavyoshauri tena wanaitwa wanasheria wakuu wa CHADEMA.Ikiwa mwansheria mkuu wa CHADEMA anaishauri CHADEMA iwe na ibara katika Katiba yake inayozuia mwanachama asiende Mahakamani kulalamika juu ya haki yake anashindwa nini kuishauri Serikali isiruhusu raia wake kuishitaki Serikali na yeyote atakayekaidi atakuwa amepoteza sifa ya uraia?
Think twice my learned brother.
Idios,
Magwayega, Leonard.

Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments