[Mabadiliko] Prof. Tibaijuka kupasua jipu leo. Je, atafuata nyayo za Werema?

Thursday, December 18, 2014

JF

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Kajumulo Tibaijuka, leo Alhamisi atarajia kukutana na waandishi wa habari saa tano asubuhi katika hoteli ya Grand Hyatt (Kilimanjaro). 

Taarifa zilizothibitishwa na Prof Tibaijuka mwenyewe, zinasema waziri huyo atazungumzia ukwapuaji wa mabilioni ya Sh. Katika akaunti ya Escrow na jinsi anavyohusishwa kunufaika nayo.

"Ni kweli nimelekeza wasaidizi wangu wizarani waniandalie mkutano na waandishi, ninataka kuzungumzia kwa kina, tuhuma ninazohusishwa kuhusu mimi kunufaika na fedha zenye utata kwente akaunti ya Escrow," alieleza Prof. Anna Tibaijuka kwa njia simu.

Prof. Anna Tibaijuka hakutaka kuingia kwa undani kuzungumzia juu mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyotaka kujiudhuru wadhifa wake wa uwaziri.

Aliishia kusema, "Wewe si mwandishi? Si umenusa na ukajua kuwa nina mkutano na waandishi habari kesho? Subiri mambo yatajulikana hapo," alisema Prof. Anna Tibaijuka huku akicheka.

mytake:naona mzee wetu muheshimiwa kuliko wote Tanzania ameshakuwa mtaalamu wa "chenga za mwili"kwasababu na yeye yupo kwenye mgao wa mlungula hivyo hawezi kuwafukuza kazi lakini alishajadiliana nao hivyo alivyotuambia "nitawawajibisha kwanzia wiki ijayo" wewe ulidhani atawawajibishaje???? ndio hivyo sasa 

swali lililobaki ni je mama tibaijuka atafwata nyayo za werema ......!!!!

muhongo na maswi ???....tusubiri

--
Unapokea Email hizi kwa sababu umejiunga na Jukwaa la 'Mabadiliko'.
Kuchangia mada tuma kwenye Email hii: mabadilikotanzania@googlegroups.com
 
 
For more options, visit this group at:
http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania?hl=en?hl=en
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Mabadiliko Forum" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to mabadilikotanzania+unsubscribe@googlegroups.com.
To post to this group, send email to mabadilikotanzania@googlegroups.com.
Visit this group at http://groups.google.com/group/mabadilikotanzania.
To view this discussion on the web visit https://groups.google.com/d/msgid/mabadilikotanzania/CACChgVRH5ex%2B_T4KRBgxpddMgc8KkGg%3Dhp%2BiqWBHzaB%2BWxWQGw%40mail.gmail.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments