Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia, amesema leo Jumatano Desemba 17, 2014, kuwa hatajiuzulu ng'o kutoka wadhifa wake kwa sababu ya kashfa ya kuvurugika kwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini Jumapili iliyopita.
Badala yake, waziri Ghasia amesema Wakurugenzi sita wa Halmashauri wamefutwa kazi, watano kusimamishwa huku wengine kushushwa vyeo baada ya kubainika kuwa walichangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, Desemba 2014.
Akitangaza hatua hiyo inayotokana na ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Ghasia amesema uamuzi huo umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Amewataja Wakurugenzi waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni wa Halmashauri za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda. Waliosimamishwa kazi ni Wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na Manispaa ya Sumbawanga.
Watatu waliopewa onyo kali ni wa Rombo, Busega na Muheza. Wengine watatu waliopewa onyo la kawaida ni Wakurugenzi hao wa Manispaa za Ilala, Hai na Mvomero.
Soma zaidi vipande vifuatavyo vya taarifa hiyo...
-- Badala yake, waziri Ghasia amesema Wakurugenzi sita wa Halmashauri wamefutwa kazi, watano kusimamishwa huku wengine kushushwa vyeo baada ya kubainika kuwa walichangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, Desemba 2014.
Akitangaza hatua hiyo inayotokana na ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Ghasia amesema uamuzi huo umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Amewataja Wakurugenzi waliotenguliwa uteuzi wao kuwa ni wa Halmashauri za Mkuranga, Kaliuwa, Kasulu, Serengeti, Sengerema na Bunda. Waliosimamishwa kazi ni Wakurugenzi wa Hanang', Mbulu, Ulanga, Kwimba pamoja na Manispaa ya Sumbawanga.
Watatu waliopewa onyo kali ni wa Rombo, Busega na Muheza. Wengine watatu waliopewa onyo la kawaida ni Wakurugenzi hao wa Manispaa za Ilala, Hai na Mvomero.
Soma zaidi vipande vifuatavyo vya taarifa hiyo...
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments