[wanabidii] Mwanamke embu tuelewe sisi wanaume, wengi wenu hamtuelewi

Thursday, December 18, 2014

Mwanamke embu tuelewe sisi wanaume, wengi wenu hamtuelewi

1. Wanaume hatuitaji ngono tu kutoka kwako:
Wanawake wengi wanaamini au kufikiria kwamba wanaume wengi wanataka sex kutoka kwao. Hii ndio inawapelekea kuingia kwenye mahusiano wakiwa wamelibeba hilo kichwani na kuamini mwanaume atafanya kitu chochote as long anapata sex. Hii siyo kweli Wanaume wengi tunapenda sex ila siyo hilo tu tunalipenda au tunalitaka katika mahusiano. Wanaume tunapenda wanawake wanao tuelewa sisi.
Yule atakaye simama na sisi kwa kutoa moyo na mawazo mpaka kufikia malengo..
Yule ambaye anaingia kwenye mahusiano na kuweka vitu sawa vile ambavyo havikuwa sawa. 
Yule ambaye atatufanya tuwe na mipangilio na maono ya badae.
Yule ambaye anakuwa na tabasamu na kicheko (mpenda matani).
Yule ambaye anaipenda familia na kuniheshime mimi kama mwanaume. Vitu vingi ni muhimu sana kuliko sex kwa sisi wanaume.

2. Pia sisi wanaume tunapenda sana kutumia pesa kwa wanawake:
Na jibu ndiyo, tunapenda sana. Pindi mwanaume akimpenda mwanamke anaweza kuvunja kibubu kuchukua pesa ambayo ndio akiba yake ya mwisho na pengine hata pesa ya kula kesho kutwa asiwe nayo. Tunawanunuliwa wapenzi wetu chips mayai, kuku robo, baga nakadhalika huku sisi tukienda kujipikia ugali dagaa na tembere mlima. Hiyo yote siyo kwa sababu sisi ni wajinga, hiyo yote ni ku mvalue mpenzi. Wanaume tunapenda kwa mali zetu ma mioyo yetu. Kwa bahati mbaya nyinyi wanawake wengi tukiwahudumia kama hivyo mnatuona sisi mabuzi na wapumbavu. Ndio imepelekea sasa sisi wanaume wengi kujiondoa taratibu katika mfumo huo wa kuhudimia. Tunatoa kila kitu kuwapeni na pengine tunazitekeleza familia zetu na ndugu zetu kuwahudumia kisha mnatuona wajinga.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments