[wanabidii] BINTI ABAKWA BAADA YA KUPEWA LIFT

Tuesday, September 02, 2014

Na Masanja Mabula –Pemba

Msichana mwenye umri wa miaka 22 mkaazi wa Mjini
Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba amefanyiwa kitendo cha
kinyama cha kubakwa na kisha kutelekezwa na dereva wa
gari lilikokuwa limempa msaada na kupitishwa sehemu
ambayo alikusudia kwenda .

Tukio hilo limetokea juzi majira ya saa kumi za jioni
katika eneo la Weni Wete ambapo msichana huyo (jina
linahifadhiwa) kubakwa na kutelekezwa kutokana na
dereva wa gari hiyo kumkimbia baada kutekeleza kitendo
hicho .

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba Shekhan Mohammed
Shekhan amesema tayari jeshi hilo linamshikilia kijana
Mohammed Kaithar Ali (45) Mkaazi wa Wete ambaye
anatuhumiwa kuhusika na kitendo hicho .
Amesema kuwa mtuhumiwa huyo ametekeleza kitendo
hicho baada ya kutakiwa kumpa msaada (lift) kwenye gari
lake na alipofika maeneo ya Weni kijana huyo alifunga
vioo vya gari lake na kisha kumtia machepe mdomoni ili
sauti yake isitoke .

Kamanda Shekhan amefahamisha kwamba msichana
aliyefanyiwa kitendo hicho amepata maumivu sehemu
zake za siri pamoja na kupata michubuko shingoni
ambayo imetokana na harakati za kutaka kujinasua ili
asifanyiwe kitendo hicho .

'Kwa kweli mtuhumiwa anadaiwa kutekeleza kitendo
hicho tayari yupo mikononi mwa jeshi la Polisi ,na
msichana aliyebakwa yuko chini ya uangalizi wa daktari
licha ya kwamba alitibiwa na kuruhusiwa kurudi
nyumbani .

Aidha Kamanda Shekhan amewataka wananchi kuwa
makini na madereva ambao sio waaminifu na kujiepusha
kuomba msaada kwa madareva wasiowafahamu ili
kuepusha kutokea kwa matenda ambayo yanaweza
kuepukika .

Akizungumzia operesheni ya kamata kamata inayofanywa
na jeshi hilo kwa madareva , Kamanda Shekhan
amefahamisha kwamba zaidi ya magari 50 yamakamatwa
na baada ya kufanyiwa uchunguzi magari 23 yamabainika
kuwa hayafai kutembea barabarani .

Amesema kuwa madareva wa magari hayo wamefikishwa
mahakamani ambapo wametozwa faini ya kati ya shilingi
elfu 80 na lakai tatu kutokana na makosa yaliyobainika
kwenye magari yao .

Amesema kuwa operesheni hiyo itakuwa ni endelevu na
ina lengo la kuhakikisha kwamba madereva , abiria
pamoja na wamiliki wa magari hizo wanatii sharia za
usalama wa barabarani bila ya kushurutishwa .
Mwisho .

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments