[wanabidii] Mahakama Yamfunga Jela Mwizi wa Nyaya za TTCL

Tuesday, September 02, 2014
[caption id="attachment_50385" align="aligncenter" width="479"]<img src="http://www.thehabari.com/wp-content/uploads/2014/09/Mmoja-wa-watuhimiwa-wa-nyaya-za-TTCL..jpg" alt="Mmoja wa watuhumiwa wa nyaya za simu. Picha hii haina uhusiano na habari hii. " width="479" height="640" class="size-full wp-image-50385" /> Mmoja wa watuhumiwa wa nyaya za simu. Picha hii haina uhusiano na habari hii. [/caption]
<strong>Na Mwandishi Wetu</strong>
<strong>MAHAKAMA</strong> ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar es Salaam imemuhukumu kwenda jela miaka minne, Shaibu Muhidin Ndina baada ya kupatikana na kosa la kuiba nyaya za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Hukumu hiyo imetolewa Agosti 25, 2014 katika mahakama hiyo na B. Mashabara baada ya mshtakiwa kutiwa hatiani kwa kosa hilo la wizi wa nyaya(cables) za kampuni ya TTCL zenye thamani ya shilingi milioni 15.

Awali akisomewa shitaka hilo, Muhidin Ndina anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 11, 2013 maeneo ya Boko Katika Wilaya ya Kinondoni kabla ya kufikishwa mahakamani na kufunguliwa kesi namba 12/2013.

"…Aliiba nyaya (cables) za thamani ya milioni 15…alitenda kosa hilo Januari 11, 2013 Boko Katika eneo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam…" ilisomeka sehemu ya hukumu ya kesi hiyo.

Uharibifu wa miundombinu ya umma zikiwemo nyaya za simu za Kampuni ya TTCL umekuwa ukishamiri maeneo kadhaa jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kubwa kwa kampuni na usu mbufu kwa wananchi na watumiaji wa huduma za TTCL.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com


__________________________________________________________
Joachim Mushi, Mhariri Mkuu wa gazeti tando la Thehabari.com
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066/ 0786 030066/ 0756 469470
Web:- www.thehabari.com  
          http://joemushi.blogspot.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments