[wanabidii] UKWELI KATIBA IMETUSHINDA , TUNGOJE SIKU NYINGINE

Sunday, August 03, 2014
Tuseme ukweli tumeshindwa safari hii kuandika katiba. Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi. Tujipange, miaka ijayo tuandike katiba mpya bora ya maridhiano. Mgogoro huu uliosababisha mchakato kushindikana umeonesha jinsi WANANCHI wanavyotumika kama silaha. Kwa upande mmoja UKAWA wanasema kurudi bungeni ni kuwasaliti WANANCHI kwani wakienda huko, wingi wa wapinzani wao utafanya katiba ipitishwe lakini ikitosa maoni ya WANANCHI. Wakilalamika baadaye, lugha itakuwa ile ile "hawa wanashangaza kwani walishiriki kutunga katiba hii, sasa wanalalamika nini"

Kwa upande mwingine wanaowapinga UKAWA wakiwemo wahariri wa magazeti kadhaa wanasema kwa UKAWA kugoma kurudi bungeni wanawasaliti WANANCHI kwa kugoma kuwaandikia katiba yao. Kwa hiyo ni WANANCHI kote kote. Swali langu; kama WANANCHI ni muhimu hivyo, basi umuhimu huo utazamwe katika misingi ya nini WANANCHI wanahitaji kiwemo kwenye katiba. WANANCHI wapendwe sana si katika watu kufanikisha mambo yao tu bali pia katika kuwasaidia wafanikishe wayatakayo

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments