[wanabidii] Taarifa ya Bodi HESLB ya nyongeza ya muda wa maombi ya mkopo

Monday, July 14, 2014
MUDA WA NYONGEZA KWA WAOMBAJI MIKOPO AMBAO HAWAKUJAZA FOMU ZA MAOMBI YA MIKOPO KABLA YA JUNI 30, 2014

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza na Umma kwa ujumla kwamba muda wa maombi ya mikopo umeongezwa kwa mwezi mmoja kutoka Julai 1, 2014 hadi Julai 31, 2014.
Bodi ilianza rasmi kupokea maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao kuanzia Aprili 23, 2014 ambapo tarehe ya mwisho wa kupokea maombi hayo ilikuwa Juni 30, 2014.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imetoa muda wa nyongeza kwa waombaji wa 
mikopo kukamilisha maombi ya mikopo katika kipindi cha siku 30, kupitia mtandao kwa anuani: http://olas.heslb.go.tz

Mwombaji wa mkopo atakayekumbana na matatizo ya kiufundi wakati wa kujaza fomu yake apige simu kwenye dawati la msaada la Bodi kupitia namba 022 550 7910 kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa saa 2.00 asubuhi hadi saa 2.00 usiku, na Jumamosi kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 10.00 jioni.

Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi hayo kwa njia ya mtandao ni 31 Julai 2014 nahakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

IMETOLEWA NA:
KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
www.heslb.go.tz

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Previous
Next Post »
0 Comments