[wanabidii] Changamoto nne za Edward Lowassa kwenda Ikulu 2015

Wednesday, July 09, 2014
1. UFISADI

Popote linapotajwa jina la EDWARD LOWASSA, Idea ya kwanza inayokuja kichwani kwa msikilizaji ni UFISADI ULIOTUKUKA, kwamba kila Watanzania wanapoikumbuka RICHMOND, wanamkumbuka LOWASSA, kwamba kila leo LOWASSA analipwa na Serikali MABILIONI YA PESA kupitia UFISADI WA RICHMOND.
Ni vigumu sana kumtenganisha LOWASSA na RICHMOND, LOWASSA ni RICHMOND na RICHMOND ndo LOWASSA, hili halikwepeki, na Watanzania sio wepesi wa Kusahau kiasi hicho,
Upo UFISADI mwingi uliofanywa na LOWASSA, katika wizara zote alizowahi kuzitumikia na nafasi zote alizowahi kuongoza, kwa sasa itoshe tu kusema LOWASSA ni KIELELEZO KIKUU CHA UFISADI WA TAIFA HILI.

2. UTAJIRI MKUBWA
Yawezekana ni Kutokana na UFISADI wake anaoufanya, lakini ukweli ni Kwamba LOWASSA ni tajiri ambaye hata hawezi kusema mali zak amezipataje pataje, pamoja na kumiliki mali nyingi hapa Tanzania, nyingi kati ya hizo akitumia majina ya watoto zake na Maswahiba zake, lakini LOWASSA ni Miongoni mwa Watanzania wanaomiliki Mali nje ya Nchi, 
Unaweza Ukajiuliza Mtumishi huyu wa Serikali wa miaka mingi aliwezaje Kumiliki NYUMBA TATU za kifahari NCHINI UINGEREZA?, NYUMBA ZA MABILLIONI YA SHILINGI, alitoa wapi utajiri huo?. 
Gazti la RAIA MWEMA NOV.2010 lilitoa MOJA KATI YA PICHA YA MAJUMBA YA LOWASSA NCHINI UINGERZA.
Leo anazunguka kugawa pesa hizi chafu makanisani na misikitini, UTAJIRI HUU UNA MASHAKA MAKUBWA. 

3. AFYA MGOGORO.
Kama kuna jambo linawatesa wapambe wa LOWASSA ni kudorora kwa AFYA yake kila kukicha,
Sio siri tena kwamba LOWASSA ni mgonjwa, 
Pamoja na jitihada zinazofanywa na wapamb wake, kumpeleka UJERUMANI kila MWEZI kupata matibabu, Kumpatia WAGANGA wa KIENYEJI, kumpeleka mpaka kwa NABII JOSHUA ili aombewe, lakini Hali ya AFYA ya LOWASSA inazidi kuwa MBOVU kila kukicha.
Sasa hivi hawezi hata kushika kikombe kwa dakika 5 mfululizo, amedhoofika mno

Juzi alikwenda KARAGWE kumtembelea BALOZI RUHINDA ambaye amepata STROKE upande mmoja wa mwili wake, 
Cha kushangaza BALOZI RUHINDA ameonekana yupo STRONG MARA DUFU kulinganisha na aliyekuja kumuona, Lowassa ameshindwa hata kutembea na mgonjwa, matokeo yak akaanguka zaidi ya mara tatu kwenye ngazi.
Jioni yake akashindwa hata kwenda kwenye Warsha aliyoandasliwa. Hii ni Hatari

Hata wapambe wake alioongozana nao ambao ni NAZIR KARAMAGI na MUSHI ambaye ni katibu wa CCM MKOA KAGERA walionyesha kufedheheka kwa namna hali ilivyokuwa.

Sasa hivi LOWASSA ameonekana kupoteza matumaini ya kugombea tena URAIS, wapambe wake hawana matumaini na Afya yake nay eye mwenyewe hana tena matumaini.

Kwa Afya ya LOWASSA hakuna muujiza utakaomuwezesha kumudu na kuhimili heka heka za kampeni za kufanya mikutano zaidi ya 10 kwa siku.

4. KUKATALIWA NA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE

Kila mmoja anaijua nafasi ya mwalimu nyerere kwenye maisha ya siasa za Tanzania.
Mwalimu Tangu zamani alionyesha kutokumkubali kabisa LOWASSA, na kwamba UTAJIRI WAKE, UBINAFSI WAKE, UFISADI wake na dhuruma zake nyingi alizozifanya zilimpelekea mwalimu kuwa hataki hata kumsikia akishika nafasi kubwa za uongozi kwenye Taifa letu.

LOWASSA, ndio mgombea pekee anayepigiwa UPATU na viongozi na wanachama wa CHADEMA na vyama vingine vya UPINZANI, sababu kuu ya kumpigia UPATU huo ni kwamba, wanaamini kuwa LOWASSA ndio mgombea pekee ambaye ni Dhaifu na mwenye Kashfa na UBADHILIFU mkubwa kwa Taifa hili hivyo kuwarahishia njia ya kumuangusha na wao kushinda dola. Ndio maana huwezi kusikia popote Dkt.Slaa ama MBOWE akimsema vibaya LOWASSA.

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments