[wanabidii] TAMKO LA VIONGOZI WA VYUO NA URAIS WA JANUARY MAKAMBA

Wednesday, July 09, 2014

Kumekua na habari zilizoenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii na vyombo mbalimbali yakiwemo magazeti,Radio na Television kwamba Viongozi wa vyuo vikuu vya Tanzania wampigia January makamba debe la Urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015 kitu ambacho siyo kweli ukweli juu ya swala hili huu hapa;

                Kuna asasi isiyokua ya kiserikali inayojihusisha na mapambano dhidi ya maradhi,ujinga na umasikini(Forum against Disease,Ignorance and Poverty kwa kifupi FDIP) yenye makao yake makuu Dar es Salaam ambayo iliitisha semina ya siku moja mkoani morogoro kwa kutuma ujumbe wa barua pepe kwa baadhi ya Marais wa serikali za wanachuo juu ya mwaliko wa semina hiyo,ambayo kwa mujibu wa mwaliko huo asasi hii ilijitambulisha kama si ya kisiasa(non-political),si ya kiserikali(non-govermantal) na isiyolenga faida(non-profit making) na pia mwaliko ule uliipambanua zaidi asasi hii kama inajihusisha na utoaji wa mafunzo ya ujasiriamali,Elimu juu ya afya,utunzaji mazingira na elimu ya uraia kwa jamii hasa kwa vijana.Mwaliko ule uliongeza kwa sasa asasi hii imejikita katika kutatua tatizo la ajira miongoni mwa vijana kwa kuandaa mpango mkakati(Project) ambao utawezesha idadi kubwa ya vijana ambao wengi wao ni wahitimu wa vyuo vikuu wanaepukana na tatizo la ajira.Kwa ujumla maudhui ya asasi hii kwa ujumla hayakuonesha kuhusika kwa asasi hii katika masuala ya kisiasa likiwemo hilo lilidoiwa viongozi wa vyuo wamepiga kura ya kumpendekeza January makamba kama mgombea Urais mwaka 2015 kitu ambacho ni propaganda tu ili kuwahadaa watanzania kwamba wasomi wa vyuo vikuu wamefikia uamuzi huo ambacho ni kinyume na katiba za serikali za serikali za wanachuo kwa kiongozi wa serikali kusimama na kutoa tamko la kumuunga mkono mtu ambaye ni mwanachama wa chama Fulani cha siasa ambapo kwa mujibu wa katiba za serikali zetu haturuhusiwi kwani serikali zetu si za vyama vya siasa.

                Semina hii iliyofanyika katika ukumbi wa Uluguru Hotel,mkoani morogoro ilikua na ajenda tofauti kabisa na zile zilizotajwa katika vyombo mbalimbali vya habari yakiwemo magazeti.Nikiwa ndiye Rais wa serikali ya wanachuo chuo kikuu katoliki cha afya na tiba(CUHAS-Bugando),mwanza nilipokea barua pepe ya mwaliko wa semina hiyo tarehe 12 agosti,2013 baada ya kuombwa anuani yangu ya barua pepe na spika wa bunge la wanafunzi chuo cha Elimu ya biashara(CBE) tawi la mwanza ambaye alikua kama mtu aliyepewa kazi ya kufikisha taarifa kwa viongozi wa vyuo vyote vya mwanza na alikua na mawasiliano ya moja kwa moja na viongozi wa asasi hii ya FDIP aliyeniomba anuani hiyo akinitaarifu kama kuna semina morogoro ili kupata uhakika wa semina hiyo ndipo nikatumiwa barua pepe na mtu aliyejitambulisha kama Francis Nduguru ambaye hata katika mwaliko ule alijitambulisha kama katibu wa asasi ile yaani FDIP.Walinisisitiza niweze kuhudkuria lakini Kutokana na wingi wa majukumu niliteua wawakilishi wa kwenda morogoro akiwemo waziri mkuu aliyetokea njia ya mbeya kwenda morogoro kwani alikua field,waziri wa katiba sheria na Bunge aliyetokea mwanza kwenda morogoro,katibu wizara ya habari na mawasiliano na spika wa Bunge waliotokea Dar es Salaam kwenda morogoro wote walikua field huko.Kwa mujibu wa wajumbe hawa ambao tayari wamenitumia nakala laini(soft copy) ya minutes za semina hiyo,ratiba ya semina ile na yote yaliyozungumzwa katika semina ile ambayo nakala zote hizo nimeambatanisha.Ajenda zilizozungumzwa ni hizi zifuatazo na si vinginevyo;

                Elimu na mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya juu.katika hili vijana walitakiwa kutoa mawazo yao juu ya mfumo wa Elimu wa Tanzania kwa ujumla na wachangiaji pia waligusia suala la mikopo mwa wanafunzi wa Elimu ya juu

                Tatizo la ajira Tanzania hasa kwa vijana ambao wengi wao ni wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali hapa nchini,maada hii nayo ilijadiliwa kwa wachokoza maada kuchokoza maada na wajumbe kujadili na kutoka na mapendekezo

                Vijana na Siasa.Ajenda hii ilijikita katika mrengo wa namna gani vijana wataweza kuhusika katika siasa ya nchi hasa katika chaguzi zijazo ukianza na ule wa serikali za mitaa mwaka ujao 2014 na uchaguzi mkuu mwaka 2015.Hapa ilijadiliwa nafasi ya vijana kwa ujumla katika siasa na chaguzi zijazo kwa ujumla.Kilichoonekana katika semina ile ni kwamba viongozi wa vyuo vikuu waliohudhuria walikua nia wachache sana na hawakufika idadi hiyo iliyotajwa na vyombo vya habari.Wengi wa wajumbe waliohudhuria walionekana ni watu waliokua wameandaliwa maalum kwa ajili ya kazi Fulani kwani kuna ambao walionekana hata hawakuwa wanachuo bali walifika pale ili kuhakikisha jambo Fulani lililopangwa linatimia.Mshanagao kwa wajumbe hasa wa CUHAS-Bugando ulianza pale ambapo ilionekana wanaingia katika ukumbi wa semina huku mwenyekiti akiwa tayari ameshaandaliwa kinyume na utaratibu kwani mwenyekiti hupendekezwa na kuchaguliwa na wajumbe ndani ya ukumbi .Pia mfumo wa kujadili maada zilizochikozwa ulikua ni wa makundi,ambapo katika kila kundi ilionekana kulikua na mamluki waliowekwa ili kufanikisha mission hiyo iliyokua imepangwa.Ilipofika katika maada ya vijana na siasa kwenye kila kundi ilionekana kulikua na mtu aliyetaka wanakundi watoke na pendekezo la kumtaja makamba kua ndiye awe mgombea urais 2015,kitu ambacho hakikuwapo katika maada na wajumbe wa makundi husika walikataa na kujikita ktk maada kama ilivyoelekeza na walitoka na mapendekezo ya namna gani vijana kwa ujumla watahusika na siasa katika chaguzi zijazo ila si kwa kutaja jina mtu yeyote kama mgombea wa uchaguzi ujao kama ndo pendekezo la vijana La hasha!!!

Ilipofika katika ajenda ya vijana na siasa na kuonekana kuna mjumbe mamluki kwenye kundi aliyetaka jina la January makamba litajwe kama ndiye mgombea urais mwaka 2015 na wajumbe kwenye kundi walilipinga hilo kwani lilikua ni kinyume na ajenda ilivyowataka wajumbe kujadili.Baada ya kila kundi kujadili kulikua na muda wa kila kundi kuwasilisha kile walichokijadili na kila kundi liliwakilishwa kile walichokijadili bila kutaja jina la mtu yeyote mbele ya wajumbe wa semina.Ratiba ilikua imepangwa kwamba baada ya chakula cha mchana(LUNCH) kulikua na muda wa wajumbe mmoja mmoja kutoa mawazo yake kwa maada zilizojadiliwa,lakini waandaaji walipoona wajumbe wanataka kuhoji jina la January makamba kutajwa ndani  ya ukumbi kinyume na maada zilivoelekeza walikiondoa kipengele hicho cha uchangiaji maada wa mtu mmoja mmoja na baada ya watu kutoka kupata chakula cha mchana waandaaji walifunga semina na kukatisha ratiba kwani ratiba ilikua inaendelea ili kuepuka maswali ya wajumbe juu ya kuonekana jina la makamba linatajwa ukumbini kinyume na maada zilivoelekeza.

                                Baada ya kuona jina la makamba linaanza kutajwa na mamluki wajumbe ndipo wakashtuka kwamba kuna kitu kilikua kianaendelea na katika uwasilishaji wajumbe wengi wakawa wananyoosha mikono ili kuweka wazi kwamba kulikua na upotoshaji Fulani,baada ya kuona wajumbe wengi wananyoosha mikono ili kuelezwa inakuaje maada hiyo inaonekana kuhusisha jina la makamba kinyume na maudhui ya maada ndipo waanadaaji wa semina ile walilazimika kufunga semina ile ili kuepuka maswali ya wajumbe kwani ilianza kubadilika katika ukumbi wa semina.

Lakini mpaka wajumbe wanatoka katika ukumbi wa semina hakuna kura yoyote iliyopigwa kumpendekeza yeyote eti kua mgombea urais,na pia katika ukumbi wa semina hapakua na wanahabari wala chombo chochote cha habari kilichofuatilia yaliyokua yakiendelea pale na kwa namna hiyo maana yake yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari yalipikwa tu na hawa watu wenye hii asasi ambayo tulivyoifuatilia asasi hii katika mitandao inaonekana hata haijasajiliwa kwani hata tulivoitafuta katika mtandao hatukupata taarifa hata moja inaitambulisha asasi hii.

Tamko lililotolewa na Rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu Mzumbe tawi la Mbeya,Theonest Theophil kwamba viongozi wa vyuo vikuu wameazimia kuzunguka nchi nzima na kuwashawishi watanzania kumuunga mkono makamba kuwania nafasi hiyo ya Urais si ya kweli,ni msimamo wake binafsi yeye kama Theonest na si msimamo wa marais wala viongozi wowote wa vyuo vikuu,wala si msimamo wa wana mzumbe tawi la mbeya kwani hawakushiriki na si msimamo wa shirikisho letu la la wanafunzi wa Elimu ya juu(TAHLISO) kwani yeye si mwenyekiti wa TAHLISO.Pia kuna vyombo vya habari  vimemnukuu kama,"akizungumza kwa niaba ya viongozi wa wanafunzi wa vyuo vikuu alitoa msimamo huo".Huyu ndugu hawezi kuzungumza kwa niaba ya viongozi wa vyuo vikuu Tanzania kwani yeye si mwenyekiti wa TAHLISO au shirikisho lingine lolote lile linalojumuisha viongozi wa vyuo vikuu vyote Tanzania wala hakuna kikao chochote kilichofanyika kwa kuhusisha Marais wa vyuo vikuu vyote nchini kumpendekeza yeye kua msemaji au mtoa misimamo kwa niaba ya viongozi wa vyuo vikuu vyote Tanzania.

Pia tamko hili si la viongozi wa vyuo vikuu Tanzania kwani tamko la viongozi wa vyuo vikuu linapaswa kutolewa na TAHLISO ambalo ndiyo shirikisho halali la wanafunzi wa Elimu ya juu ni si vinginevyo.Pia semina hii haikuitishwa na TAHLISO na TAHLISO kama shirikisho haliwezi kutoa msimamo wa kitu ambacho haijahusika hata katika kuandaa

January makamba amekua akijipenyeza hata katika TAHLISO kwa kutumia baadhi viongozi wa vyuo vikuu ambao wamekubali kutumika.Mfano katika kongamano la Baraza la katiba lilifanyika mzumbe tawi la mbeya,terehe 2 na 3 agosti,2013. ambapo viongozi wa vyuo vikuu tulikutana ili kutoa maoni juu ya rasimu ya katiba kama ulivoagiza waraka wa tume ya mabadiliko ya katiba ya jaji warioba.Katika kongamano lile kama TAHLISO ilitakiwe tutoe maoni yetu na baadaye tutoe tamko juu ya mapendekezo yetu katika rasimu ya katiba.Ilisemekana January makamba alisafiri hadi mbeya na kukutana na baadhi ya wajumbe wa TAHLISO ambao alikaa nao usiku wa tarehe 2 kuamkia 3 agosti,ilisemekana alitaka apenyeze suala la umri wa Urais ili tamko litakalotoka TAHLISO liseme linapendekeza umri wa Urais kua miaka kati ya 30 na 35 ili kumpa yeye nafasi ya kutimiza azma yake ya kuutaka Urais.lakini hakufanikiwa kwani kongamano lile halikuhitimishwa ila lilifikia sehemu tu ya mikakati yake na ikatakiwa lingine lifanyike baadaye ili kukamilisha utoaji maoni na kutolewa tamko la TAHLISO na mapendekezo yake juu ya rasimu ya katiba mpya.Katika kongamano la Mbeya kuna viongozi ambao walipigiwa simu na mtu aliyewataka waende katika hotel fulani pale mbeya kukutana na January makamba kuna mambo anataka kuzungumza nao,kuna mtu ambaye anafahamika kama Tibaigana wanaomfahamu wanasema ni motto wa Alfred Tibaigana aliyekua kamanda wa Polisi mabaye hata katika hiyo workshop ya morogoro alijitambulisha kama mkurugenzi wa ile asasi ya FDIP iliyoitisha workshop pale morogoro.Mtu huyu alionekana pia katika lile kongamano la katiba la TAHLISO lililofanyika Mbeya,inaonekana yupo katika huo mtandao wa Rais wa serikali ya wanafunzi chuo cha Mzumbe tawi la Mbeya ambao wanaonekana kutumika na Januari makamba katika azma yake uchwara ya kuutaka Urais kwa hali na mali wakati na umri usiomruhusu kupata nafasi hiyo kwa sasa.Nimeambatanisha la nakala laini(soft copy) ya barua ya mwaliko na Ratiba ya workshop hiyo.

 

Wajumbe waligharimiwa

Nauli  walipewa Tsh.50,000/= kwenda na Tsh.50,000/= kurudi kwa waliotoka mbali na morogoro

Nauli waliotoka Dar walipewa Tsh.7,500/= kwenda na Tsh.7,500/= kurudi

Posho Tsh.70,000/=

Gharama za chakula na malazi

By;

Moses Leonard Mdede

Rais serikali ya wanafunzi chuo kikuu katoliki cha afya na tiba-Bugando(CUHAS-Bugando),Mwanza.

Phone no.0765 815179

Email address;Mosesleonard@rocketmail.com

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments