[wanabidii] UCHAGUZI SIMBA WAPINGWA KORTINI

Tuesday, June 24, 2014
UCHAGUZI SIMBA WAPINGWA KORTINI
Na Happiness Katabazi
WANACHAMA wa Tatu wa Timu ya Soka ya Simba, Jana walifungua Kesi Katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam, wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya Muda ya Kuzuia kufanyika kwa uchaguzi Mkuu wa Timu hiyo ambao umepangwa kufanyika Juni 29 Mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya Madai ya Maombi hayo madogo, Na.291/2014 yaliyofanyika chini ya hayo ya dhati la, saa nane mchana mahakamani hapo na wanachama watatu ambao ni Josephat Waryoba, Said Lly Monero na Hassan Hassan wanatetewa na Wakili wa kujitegemea Revocatus Kuuli ambao wanamshitaki Rais wa Timu ya Simba, Ismail Aden Rage na Bodi ya Udhamini ya Timu hiyo.

Kwa mujibu wa hati hiyo inayonyesha walalamikaji wana jumla ya Madai matatu ambayo dai la kwanza wakiomba Mahakama hiyo itoe amri ya kuwazuia wadaiwa kuitisha uchaguzi Mkuu uliofangwa kufanyika Juni 29 Mwaka huu.

Wakili Kuuli analitaja ombi la pili ni wanaomba jumla ya wanachama 66 waunganishwe Kwenye Kesi hiyo ili nao wawe walalamikaji dhidi ya wadaiwa kwasababu wadaiwa ambao Rage na Bodi ya Wadhamini wamevunja Katiba ya Simba , taratibu za uchaguzi na na maadili ya uchaguzi , kadi za uanachama za wanachama hao zimearibiwa.

Wakili Kuuli alidai kuwa mdaiwa wa kwanza Kamati ya Utendaji ya simba walishindwa kuweka sawa Kamati ya Maadili ya simba Kama inavyotakiwa na Katiba ya Timu hiyo na Kanuni za uchaguzi za TFF.

Alidai Kwa vitendo hivyo wadaiwa hao wamevunja taratibu zote za uchaguzi na kwamba Hakuna Chombo Cha klabu ya Simba ambacho kimepewa madaraka ya kusimama a masuala ya rufaa ya Maadili ya wanachama wake na kwamba rufaa zote zote zinazohusu Maadili zinasimamiwa na mdaiwa wa pili(Bodi ya wadhamini ya simba), nakwasababu hiyo wanaiomba Mahakama hiyo itafsiri Hilo.

" Japo Kuwa maelekezo toka TFF kwenda mdaiwa wa kwanza (rage) ya
Yaliyomtaka Rage aweke sehemu ya Kamati ya Maadili , Rage alishindwa kutekeleza maelekezo hayo KWA Madai Kuwa robo Tatu ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Timu hiyo , wanatuhumiwa KWA makosa ya utovu wa Maadili .

" Barua ya TTF kwenda KWA Rage ya Mei 29 Mwaka huu ,na barua ya Mwenyekiti wa Simbaya Juni 17 Mwaka huu ambayo alikuwa akimjibu Rais wa TFF, Jamal Malinzi ni ambazo tumeziambatanisha katika hati yetu ya madai kama vielelezo ili mahakama itoe tafsiri ya sheria " alidai wakili huyo.

Aidha walalamikaji hao wanadai Kuwa Kamati ya Uchaguzi ya Simba ipo kinyume na Katiba ya Timu ya Simba Kwani Kamati hiyo Ina baadhi ya wanachama ambao walioteuliwa Na Kamati ya Utendaji na waliondolewa na Rais wa Timu hiyo Katika Kamati hiyo kinyume Cha Sheria .

Pia wamedai Kuwa Kamati ya uchaguzi ya simba haina mamlaka ya Kamati ya Maadili ya kuwandoa baadhi ya wagombea Katika mchakato wa uchaguzi Mkuu Kwani Kamati ya uchaguzi wa kuwachuja wagombea pekee na suala la utovu wa Maadili na nidhamu ya mgombea jukumu Hilo limekabidhiwa Kwenye Kamati ya Maadili peke na siyo Kamati ya Uchaguzi .

"Kwa Sababu hiyo tunaimba Mahala hii itamke Kuwa utaratibu wote wa kuendesha uchaguzi ndani Timu ya Simba ni batiri kwasababu umekiuka Katiba ya Simba" Alidai Wakili Kuuli.

Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Juni 24 Mwaka 2014








Sent from my iPad

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com

Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma

Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments