YAH: TAMKO LA MEWM KULAANI HUJUMA ANAZOFANYIWA EDWARD N. LOWASA NA KAMATI YA MAADILI YA CCM NA MWENYEKITI TAIFA
Umoja wa Marafiki wa Mh Edward N. Lowasa Wasio na Mipaka unaundwa na wanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi ndani na nje ya nchi, pia wapo mawaziri na makada viongozi wa ccm mikoa, wilaya, majimbo, kata na matawi, pia wapo wasio wanachama na wanachama wa vyama vingine nchini.
Sisi marafiki wa Mh Lowassa Tusio na Mipaka tulikutana usiku wa kuamkia leo, tunapenda kutoa tamko kulaani kamati ya maadili ya Chama chetu na Mwenyekiti wa CCM taifa, Mheshimiwa Rais Wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuonyesha waziwazi kumhujumu Mh Edward Lowasa asitimize ndoto yake.
Kamati ya maadili ya Chama mwezi wa nne mwaka huu, iliwasimamisha makada wa CCM walioonyesha kuwa kwenye harakati za kuwania kuteuliwa kugombea Urais 2015 kwa mda wa miezi 12, akiwemo rafiki yetu Mh Lowasa.
Lakini katika hali ya kusikitisha baadhi ya makada wanapewa fursa za kuendelea kupiga kampeni mbele za umma bila kamati kukemea kwakutumia mwavuli wa mwenyekiti wa Chama.
Umoja wetu wa Marafiki wa Mh Lowasa Tusio na Mipaka tunahoji, hii ndio sababu iliyofanya mkatae hoja yetu kwenye mkutano mkuu Dodoma?
Pia tunahoji tena, gharama hizi kubwa zinazotumia kufadhiri vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia chama chetu zinatoka wapi? Na zimekuwa na faida gani kwa chama chetu tangu 2010?
Tunatoa Siku thelathini(30) kuanzia leo 24/06/2014, Chama chetu cha CCM kwakutumia kamati zake inaondoa ukakasi huu katika Chama, Ikiwa Mwenyekiti na ccm kwa ujumla watapuuza, Sisi Marafiki wa Mh Lowasa Tusiokuwa na Mipaka, tutachukua maamuzi magumu yatakayo kigharimu chama chetu, na kulinusuru Taifa.
Sisi wana CCM , tunapenda kuwahimiza watanzania popote pale walipo duniani kushirikiana nasi katika mapambano ya kudai haki ya kuchagua na kuchaguliwa ndani ya Chama chetu kama ilivyokuwa mila na destuli ya chama chetu.
Tuna imani Chama Makini Cha CCM kitaongoza Mchakato wa kumpata rais bora hapo 2015 ilimradi haki itendeke, vinginevyo tutagawana mbao.
Ahsanteni,
Imetolewa Dar Es Salaam.
Mtuya M. Lugola
Mwenyekiti wa Marafiki wa Mh Lowasa Wasio na Mipaka CCM,
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments