Serikali imeagiza gazeti la Mawio kueleza sababu za kupotosha na kukejeli nia njema ya serikali kwa wananchi wake kuhusu Hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Akizungumza jana, Mkurugenzi Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema gazeti hilo la wiki linatakiwa kujieleza ndani ya siku tatu. Alisema mbali na kujieleza, gazeti hilo limepewa siku saba hadi
Aprili 23, mwaka huu, kukanusha taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Mwambene, katika gazeti hilo toleo na 0091 la Aprili 17-23, mwaka huu lenye kichwa cha habari 'Hati za Muungano utata,' taarifa husika inakebehi hati hiyo na kujenga taswira kwamba ni ya kughushi na batili. Linadai waandishi wawili ndiyo waliona kati ya waandishi zaidi ya 20 waliokuwepo kwenye mkutano wa Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
"Taarifa ya gazeti la Mawio ni ya kimawazo na imeandikwa pasipo shaka kutimiza malengo na maslahi binafsi wanayojua," alisema Mwambene.
Alisema pamoja na maelezo ya Katibu Kiongozi, Sefue, gazeti hilo liliamua kwa utashi wake kukejeli na kuuaminisha umma wa Watanzana kwamba Hati ya Muungano ina utata.
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.
0 Comments