[wanabidii] Ni ukosefu wa adabu kuwatukana waasisi wa Tanzania - JK

Friday, April 18, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ni ukosefu wa adabu kuwatukana waasisi wa Tanzania - JK

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu kuwa baadhi ya Watanzania kuwatukana, kuwadhihaki na kuwakejeli Waanzilishi ma Taifa la Tanzania, Hayati Julius Nyerere na Hayati Sheikh Abeid Amaan Karume. 

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa viongozi hao wawili wameifanyia Tanzania mambo mengi, mambo makubwa na mambo ya kihistoria kiasi cha kwamba Watanzania wanao wajibu wa kudumisha na
kuenzi heshima yao kwa namna ya kudumu. 

Akizungumza na Wahariri wa baadhi ya vyombo vya habari usiku wa jana, Jumatano, Aprili 16 katika mahojiano maalum ya kuadhimisha Miaka 50 ya Muungano, Rais Kikwete amesema: "Ni kukosa adabu na ni utovu mkubwa wa nidhamu kwa Mtanzania yoyote kuwatukana, kuwadhihaki ama kuwakejeli waasisi wa Tata letu. Hawa ni watu ambao waliifanyia nchi yetu mambo makubwa," amesema Rais Kikwete na kuongeza: 

"Mzee Karume yule aliongoza Mapinduzi yaliyoondoa dhuluma na uonevu pale Visiwani. Waafrika walio wengi walikuwa wanaonewa sana pale Tanzania Visiwani, pengine watu wamesahau, lakini hata pale walipokuwa wanashinda uchaguzi bado walikuwa hawapewi nafasi ya kuongoza maisha yao wenyewe." 

Amesisitiza Rais Kikwete: "Ni ukosefu wa adabu kwa yoyote kumshutumu mtu aliyejitolea kiasi hicho ili kubadilisha mfumo dhalimu na kujenga maisha na mazingira ya maisha bora kwa wengi." 

"Mzee Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye umoja, lenye amani na mshikamano. Misingi ambayo aliijenga yeye ndiyo imeendelea kuongoza Taifa letu kwa miaka pate hii. Viongozi wengine wale ambao wamemfuata yeye — Mzee Mwinyi, Mzee Mkapa na sasa mimi mwenyewe, tumefuata na kuongozwa na misingi hii. Na siku nchi yet inaamua kuipuuza misingi hiyo, tutaingia katika matatizo makubwa." 

Rais Kikwete ametoa msimamo boo baada ya kuwa ameulizwa kuhusu matusi, kejeli, dhihaki ambazo zimekuwa zinaonyeshwa na wajumbe wachache ma Bunge Maalum la Katiba juu ya waasisi hao ma Tanzania na Wabunifu Wakuu wa Muungano wa Tanzania. 

Imetolewa na: 
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM, 
17 Aprili, 2014 

--
Send Emails to wanabidii@googlegroups.com
 
Kujiondoa Tuma Email kwenda
wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com Utapata Email ya kudhibitisha ukishatuma
 
Disclaimer:
Everyone posting to this Forum bears the sole responsibility for any legal consequences of his or her postings, and hence statements and facts must be presented responsibly. Your continued membership signifies that you agree to this disclaimer and pledge to abide by our Rules and Guidelines.
---
You received this message because you are subscribed to the Google Groups "Wanabidii" group.
To unsubscribe from this group and stop receiving emails from it, send an email to wanabidii+unsubscribe@googlegroups.com.
For more options, visit https://groups.google.com/d/optout.

Share this :

Related Posts

0 Comments